Mwanafunzi wa Sekondari Atiwa Mbaroni Akiwa na Kete 24 za Cocaine..!!!
Polisi mkoani Mbeya wametangaza kumkamata mwanafunzi anayesoma sekondari akiwa na kete 24 za cocaine eneo la Mbalizi mkoani Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoa, Dhahir Kidavashari amesema Jumanne hii kuwa polisi wamemkamata mwanafunzi huyo akiwa anaziuza dawa hizo kwa watu mbalimbali na kwamba upelelezi wa kuwadaka mapapa unaendelea.
Kukamatwa kwa kijana huyo kunatokea siku moja baada ya Rais John Magufuli kuunga mkono kazi ya Makonda huku akiwaagiza wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia wote wanaojihusisha na dawa za kulevya bila kujali huyu ni nani.
Kidavashari amesema kwamba vita dhidi ya dawa za kulevya ilikuwa ikiendelea, lakini sasa imepata msukumo mpya ambao unalenga kuukata mnyororo mzima wa mtandao unasambaza dawa hizo.
Mwanafunzi wa Sekondari Atiwa Mbaroni Akiwa na Kete 24 za Cocaine..!!!
Reviewed by Unknown
on
08:59:00
Rating:
Hakuna maoni: