Kweli Kufa Kufaana,Ray C Aamua Kuja na Kamapeni Hii Wakati Wema na Wenzake Wakiwa Ndani Kwa Kuhusishwa na Madawa ya Kulevya..
MSANII wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila maarufu kama‘Ray C’ Kiuno Bila Mfupa, amejitokeza kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kuweka video mtandaoni ikimuonesha mtu aliyepoteza maisha kwa madawa ya kulevya huku akiandika: “SAY NO TO DRUGS”
Aidha Ray C ambaye anatajwa kama nimhanga wa madawa hayo aliwahi kupewa huduma vituo mbalimbali vinavyotoa huduma kwa waathirika wa madawa ya kulevya ‘Sober House’ na baada ya muda anaonekana kurudia hali ya kudhoofu na kuwa kama mhanga wa madawa hayo.
Ray C amewahamasisha watu wengi kupitia video aliyoiweka katika mtandao na imewagusa Watanzania wengi kwa kuchangia maoni yao juu ya athari mbaya za madawa ya kulevya na sakata la linalonguruma kwa sasa nchini.
Kweli Kufa Kufaana,Ray C Aamua Kuja na Kamapeni Hii Wakati Wema na Wenzake Wakiwa Ndani Kwa Kuhusishwa na Madawa ya Kulevya..
Reviewed by Unknown
on
09:02:00
Rating:
Hakuna maoni: