Obama kuvunja rekodi iliyoachwa na Rais wa 28 wa Marekani, Woodrow Wilson
Tayari Marekani imepata rais mteule, Donald Trump ambaye atachukua nafasi ya Rais Barack Obama na tayari Obama ameanza kufanya maandalizi ya nyumba ambayo atahamia baada ya muda wake wa kukaa madarakani kumalizika.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo Barrack Obama na familia yake wametafuta nyumba jijini Washington ili kumwezesha binti yao Sasha kumaliza masomo yake.
Imeelezwa kuwa Obama na familia yake wamejipatia jengo zuri katika maeneo ya Kalorama yaliyopo Washington DC kiasi cha maili mbili tu kutoka walipokuwa wanaishi mwanzo, Ikulu.
Rais mwingine ambaye alibaki ndani ya Washington DC alikuwa ni Woodrow Wilson mwaka 1921.
Kwa kawaida marais wengi wakimaliza ngwe yao walikuwa wakiukimbia mji huo na kwenda kuishi maeneo ya mbali kabisa.
Maeneo ya Kalorama hukaliwa zaidi na balozi mbalimbali kwa hiyo kuna usalama unaotakiwa kwa kiongozi huyo anayestaafu wa Marekani.
Imeelezwa kuwa kasri hilo lenye vyumba tisa vya kulala, mabafu manane ni mali ya aliyekuwa mwandishi wa rais wakati wa utawala wa rais Bill Clinton Joe Lockart na mkewe Giovanna Gray, ambao walilinua kwa dola za Marekani milioni 5.3 mwaka 2014.
Kasri hilo lipo katika eneo la futi za mraba 8,200 na lilijengwa mwaka 1928 na kufanyiwa maboresho kadhaa ndani.
Angalia picha za kasri hilo ambalo akina Obama wanataraji kuishi kuanzia Januari mwakani.
Obama kuvunja rekodi iliyoachwa na Rais wa 28 wa Marekani, Woodrow Wilson
Reviewed by Unknown
on
21:00:00
Rating:
Hakuna maoni: