Auawa Kwa kukatwakatwa Mapanga Wilayani Songea

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Severin Mgogo mwenye umri wa miaka 80 ameuwawa kwa kukatwa katwa na mapanga na mmoja Antony Ndauka kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika wakituhumiwa kuwa washirikina tukio hilo limefanyika hivi karibuni katika kijiji cha Nakahegwa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Gofrey Nilahi anataarifa Zaidi.
Afisa tarafa ya Mhukuru Salma Mapunda amesema kuwa kabla ya tukio hilo la kinyama watu hao waliwahi kuzingirwa nyumbani kwao hali iliyomlazimu mtendaji wa kijiji cha Nakahegwa kukodi pikipiki na kuwapakiza wote wawili usiku wakiongozwa na mgambo wa kijiji kuwapeleka kituo kidogo cha polisi kata ya Magagula kabla ya kufika kundi la watu wakiwa na mapanga waliwavamia na kuanza kuwapiga ambapo Mzee severin Mgogo alipoteza maisha na Antony hali yake ni mbay yupo hospitali ya misheni Peramiho.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti Mgema ametembelea kijijini hapo na kufanya mkutano wa hadhara amemwagiza mkuu wa kituo cha polisi kuwakamata viongozi wa kijiji mwenyekiti na kamati yake hatimaye hatua za kisheria zichukuliwe kwa kosa la kushindwa kutatua tatizo hilo kwa wakati.
Mtoto wa marehemu John Mgogo ameiomba serikali kuchukua za haraka za kuwasaka waliofanya tukio hilo.
Auawa Kwa kukatwakatwa Mapanga Wilayani Songea Auawa Kwa kukatwakatwa Mapanga Wilayani Songea Reviewed by Unknown on 02:39:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.