Dawa Nyingine za kulevya zakamatwa Mabwepande
Watu 4 wamekamatwa na misokoto 16 ya bangi ambapo nyingine ikiwa imesagwa na nyingine ikiwa imevunwa nyumbani kwa Bi Hadija Mwinyi Mkuu kufuatia msako wa nyumba kwa nyumba uliousisha jeshi la polisi na viongozi kata ya Mabwepande na kata ya Bunju manispaa ya Kinondoni jijini Dar-es-Salaam.
Msako huo umekuja baada ya serikali kupiga vita na kupambana na wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya,uvutaji unga na bangi huku wakifanikiwa kukamata watu 4 ambao wamekutwa na bangi na vitu mbali mbali na mmoja kufanikiwa kukimbia ambapo wenyeviti wa serikali za mitaa katika kata hizo wakiomba wananchi kutoa ushirikiano ili kuwafichua na kukomesha biashara hizo.
Diwani wa kata ya Bunju Bw. Heri Nasoro amesema wameadhimia kufanya msako huo kila siku kwa kushirikiana na jeshi la polisi ili kuondoa kabisa mlipuko wa vijana wengi katika kata na mitaa Bunju walioathirika na madawa haya ambapo wananchi wamepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ili kuokoa vijana wengi wanaojiusisha na biashara hiyo.
Dawa Nyingine za kulevya zakamatwa Mabwepande
Reviewed by Unknown
on
02:40:00
Rating:
Hakuna maoni: