Walimu wakatwa Mapanga na watu wasiojulikana Musoma

Walimu wawili wa shule ya msingi ya Kwibara ‘B’ katika Halmashauri ya Musoma vijijini mkoani Mara,wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara mjini Musoma baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana baada ya kuwavamia nyumbani kwao wakiwa wamelala.

Wakizungumza baada ya kufikishwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara,walimu hao wamesema walikatwa mapanga hayo baada ya milango yao kuvunjwa kisha kupambana na watu hao kabla ya kuanza kuwashambulia kwa mapanga huku mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Bw Swedy Elias,akisema tukio hilo limetokea majira ya saa saba usiku.

Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Musoma SSP Renatus Chalya,akizungumza na wananchi wa kijiji hicho baada ya tukio hilo kutokea,pamoja na kulaani vikali vitendo hivyo vya uvamizi dhidi ya watumishi wa umma,amesema Jeshi la polisi litachukua hatuka kali katika kukomesha vitendo hivyo.
Walimu wakatwa Mapanga na watu wasiojulikana Musoma Walimu wakatwa Mapanga na watu wasiojulikana Musoma Reviewed by Unknown on 02:41:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.