Nikki wa Pili Atoboa Siri ya Kilichomvutia kwa Mpenzi wake Mpaka Kumvisha Pete

Nikki wa Pili Atoboa Siri ya Kilichomvutia kwa Mpenzi wake Adikumvisha Pete
Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili ameweka wazi kitu cha kipekee kilichomvutia kwa mpenzi wake Joan, hadi kufikia hatua ya kutangaza ndoa.


Akizungumza na www.eatv.tv, Nikki amesema kwamba upendo wa kipekee aliooneshwa na mwanamke huyo ndiyo kitu cha kipekee kilichomnasa, na kufanya awaache wanawake wote warembo bongo na kutua kwake.

“Kwanza ananipenda, hicho ni cha kwanza, lakini cha pili tunaweza kuelewana, ikiwa ni kwenye makosa, kupatia , kuumia, kufurahi, na yeye anaweza kuelewa hapa Niki yupo hivi kwa sababu hii, na ananielewa, lakini pia anaelewa kuwa Nikki ana mazuri yake mengi na mabaya yake, kitu ambacho kinapungukia kwangu anaweza kukijazia,” amesema Nikki.

Nikki wa pili na mpenzi wake Joan wamekuwa kwenye mahusiano kwa zaidi ya miaka miwili, na hivi karibuni ameamua kumchumbia rasmi, ikiwa ni mwanzo wa safari yao ya maisha ya ndoa.
Nikki wa Pili Atoboa Siri ya Kilichomvutia kwa Mpenzi wake Mpaka Kumvisha Pete Nikki wa Pili Atoboa Siri ya Kilichomvutia kwa Mpenzi wake Mpaka Kumvisha Pete Reviewed by Unknown on 13:19:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.