HII NDIYO WILAYA YENYE IDADI KUBWA YA MAKAHABA...DANGURO KUBWA ZAIDI LABORESHWA

Ikisemekana kuwa wilaya yenye idadi kubwa zaidi ya mahahaba bara Asia, Sonagachi ni wilaya yenye mitaa yenye barabara nyingi nyembamba na njia za uchochoroni kati kati mwa jiji la Kolkata, ikiwa ni makazi ya makahaba takriban 11,000.
Wakifanya kazi kwa ushirikiano na wasanii wenye makao yao Bangalore, wasanii wa michoro wasiokubali maumbile yao ya jinsia (transgender) walichora michoro kwenye michoro ya rangi za kuvutia kwenye baadhi ya majengo kama sehemu ya kampeni ya kuhamasisha umma kuhusu haki za makahaba na pia kujaribu kuzuia unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Uchoroji wa michoro hii ulichukua muda wa wiki nzima
Mengi kati ya madanguro haya yamechakaa
Kuta katika mtaa wenye majengo yaliyosongamana pia zilipakwa rangi.
Kuna mipango ya kuyapaka rangi majengo zaidi katika wilaya ya Sonangachi.
Ukahaba umesalia kuwa tatizo kubwa kwa India, ambako wanawake milioni tatu wanaaminiwa kufanya biashara ya ukahaba.

Picha hiyo inaonyesha mchoro uliochorwa kwenye jengo la chama cha ushirika cha makahaba.

Hapa wapitanjia na wafanyabiashara wanaonekana kwenye moja ya jengo lililopigwa rangi.
.
Wapita njia wa Kihindi wakipita kwenye mtaa wa madanguro ya makahaba yenye michoro katika wilaya ya Sonangachi jijini Kolkata

HII NDIYO WILAYA YENYE IDADI KUBWA YA MAKAHABA...DANGURO KUBWA ZAIDI LABORESHWA
Reviewed by Unknown
on
04:42:00
Rating:
Hakuna maoni: