TID Ampachika Mimba Mwanamuziki Recho...Mwenyewe Aruka Viunzi...

Msanii Khalid Mohamed maarufu kwa jina la TID, ameruka viunzi na kukana tetesi za kumpachika ujauzito msanii mwenzake Rachel.

Akizungumza kwenye kipindi che eNewz kinachorushwa na East Africa Television, T. I. D amesema kwa sasa hatarajii mtoto yeyote na mwanamke yeyote, na kwamba habari hizo hazina ukweli.

“Hapana, sitarajii mtoto yeyote na Rachel, sina mimba ya Rachel, siyo kweli bwana, hamna mtu mwenye mimba wala nini, kila mtu anataka kuwa na mimba ya Mnyama, sasa wanawake wangapi wanataka kuwa na ujauzito wa mtoto wangu?”, alisikika T. I. D

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa wasanii hao wana mahusiano ya kimapenzi, zilizoibua habari kuwa Rachel ana ujauzito wake
TID Ampachika Mimba Mwanamuziki Recho...Mwenyewe Aruka Viunzi... TID Ampachika Mimba Mwanamuziki Recho...Mwenyewe Aruka Viunzi... Reviewed by Unknown on 22:46:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.