MSANII MSAGA SUMU ADAI ALIJUA KUWA MUZIKI WA SINGELI UTAKUFA

Tokeo la picha la msaga sumu
Msaga Sumu amefunguka na kusema alitambua mapema kwamba aina ya muziki wanaofanya utakufa mapema kwani wasanii wake hawana ushirikiano.

Msaga Sumu amesema kwamba wasanii wachanga waliokuja kuibuka hivi karibuni ndio chanzo cha kupelekea singeli kupotea kwani walianza kutengeneza mabifu wao kwao badala ya kuboresha kazi.
"Nilijua muziki wa Singeli utakufa kwa sababu hatukuwa na ushirikiano, wenzetu wa bongo fleva wamefanikiwa sana mpaka wamejijengea majina makubwa ni kwa sababu wameweza kushikamana, Tatizo pia hawa watoto waliokuwa wametamba na nyimbo zao mbili mbili nao wakaanza kuwekeana mabifu na mwisho wa siku wamepotea wao walidhani wamemaliza", Msaga amesema.
Akizungumzia kwa upande wake kushindwa kuachia nyimbo mfululizo, Msaga Sumu amesema 
"Mimi niliacha kutoa nyimbo baada ya kuona tena kuna kuigana. Wasanii wanashindwa kuwa wabunifu kwa sababu na badala yake wote tukawa tunaonekana hatuna kitu chochote" aliongeza Msaga Sumu
MSANII MSAGA SUMU ADAI ALIJUA KUWA MUZIKI WA SINGELI UTAKUFA MSANII MSAGA SUMU ADAI ALIJUA KUWA MUZIKI WA SINGELI UTAKUFA Reviewed by Unknown on 22:20:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.