Video, Jay Z msanii wa kwanza wa hiphop kwenye Songwriters Hall of Fame, Obama ampa hongera…
Jay Z amekuwa msanii wa kwanza wa hiphop kupewa heshima ya Jina lake kuwekwa kwenye Songwriters Hall of Fame.
Staa huyu wa hiphop ametumia twitter yake kushukuru mashabiki na wadau wote waliompa ushirikiano mpaka kupata mafanikio haya.
Jay Z amewataja wasanii kama Rakim, 2Pac, Notorious B.I.G., Nas, J. Cole,Kanye West, Kendrick Lamar, Chance the Rapper, Lauryn Hill, Nicki Minaj,De La Soul, Eminem na wengine wengi.
Jay Z hakuwepo kwenye shughuli hio ya kupokea heshima hio kutokana na hali ya mke wake ambaye ni mjamzito akitegemea kujifungua mapacha.
Aliyepokea heshima hio kwa niaba ya Jay Z ni Katibu mtendaji wa Warner/Chappell Jon Platt,
Rais Barack Obama pia amempa hongera Jay Z na wasanii wengine waliopata heshima hii katika Songwriters Hall of Fame mwaka huu kama Babyface, Berry Gordy, Jimmy Jam & Terry Lewis, Max Martin na wengine wengi.
Video, Jay Z msanii wa kwanza wa hiphop kwenye Songwriters Hall of Fame, Obama ampa hongera…
Reviewed by Unknown
on
05:13:00
Rating:
Hakuna maoni: