Hii Ndio Ndinga Anayomiliki Harmorapa
Harmorapa sio mtu wa mchezo mchezo, unafahamu gari analolimiliki?
Kupitia kipindi cha Top 20 cha EA Radio, rapper huyo amesema kuwa anamiliki ndinga aina ya Nissan Morano na mwaka jana meneja wake ndio aliyempeleka katika shule kwa ajili ya kujifunza udereva.
“Mwaka jana nilipotoa ngoma yangu ‘Usigawe Pasi’ bosi wangu akaniambia naona ipo siku utakuwa staa hivyo akanisaidia kunipeleka driving school ilinijifunze kuendesha gari. Nashukuru Mungu sasa najua na naendesha gari ya Nissan Morano,” amesema Harmo.
“Pale home kuna magari mengi tu ndio maana naendesha tofauti tofauti, ila hilo la Nissan Morano ndiyo alilonipa kama zawadi Meneja wangu mwaka jana,” ameongeza
Hii Ndio Ndinga Anayomiliki Harmorapa
Reviewed by Unknown
on
05:17:00
Rating:
Hakuna maoni: