Mlinzi wa zamani wa 2 Pac ataja watu waliohusika kwenye kifo cha 2 Pac…ni kutoka kundi gani na kwanini walikuwa na beef nae….

Sababu ya 2Pac kupigwa risasi na ugomvi uliotokea ndani ya ukumbi wa pambano laMike Tyson mjini Las Vegas.
Hii ni kwa mujibu wa mlinzi wa zamani wa 2 Pac na Suge Knight ambaye anasema alikuwepo usiku huo 2 Pac anapigwa risasi.
Blood Piru OG Mob James anasema Kijana kutoka kundi la wahuni la Crips alikanyagwa na 2 Pac walivyokuwa kwenye ukumbi wa MGM Grand mjini Vegas wakati wa pambano la Tyson, 2 Pac hakuomba msamaha na walibadilishana maneno makali, pia Suge Knight hakutaka kuamua ugomvi ndio maana vijana hao waliondka kwa hasira na baadae kumpiga risasi 2 Pac“. 
Blood Piru OG Mob James ambaye alikuwa karibu na Suge Knight boss wa Death Row Records kijana kutoka The South Side Crips ndio alifyatua risasi.
Piru amezidi kulaumu uongozi mbovu wa Suge Knight akidai ata wahuni waliotakiwa kumlinda 2 Pac hawakuwa wanalipwa vizuri na Suge Knight ndio maana ilionekana ni rahisi kumdhuru 2 Pac.
Tupac alipigwa risasi Masaa mawili baada ya kutofautiana na wahuni hao wa Crips, Pac na Suge walikuwa wakielekea kwenye club maarufu ya 662.
Piru anasema Suge Knight ni shetana sababu ata kaka yake alifariki kutokana na yeye kujihusisha na lebo hio ya Death Row na mmiliki wake Suge Knight.
Mlinzi wa zamani wa 2 Pac ataja watu waliohusika kwenye kifo cha 2 Pac…ni kutoka kundi gani na kwanini walikuwa na beef nae…. Mlinzi wa zamani wa 2 Pac ataja watu waliohusika kwenye kifo cha 2 Pac…ni kutoka kundi gani na kwanini walikuwa na beef nae…. Reviewed by Unknown on 00:31:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.