Maneno makali ya Wema Sepetu matumizi na uuzaji wa dawa za kulevya…
Wema Sepetu ameweka jambo moja wazi na lieleweke kuwa yeye sio Mtumiaji wa Muuzaji wa dawa za kulevya. Kupitia App yake mpya ya #WemaSepetu ametoa kauli hii baada ya kuwemo kwenye orodha ya majina ya watu maarufu wanaotumia dawa za kulevya kutoka kwa Mko wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa orodha ya mastaa Wema Sepetu, TID, Mr Blue, Chidi Benz, Recho na wengine kujisalimisha kwenye kituo cha polisi central jijini Dar, Ijumaa hii kwa mahojiano zaidi.
Kupitia video kwenye #App Yake Wema anasema “Mimi kama Wema nimekuwa nikisemwa sana kuhusu kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na hata kujihusisha katika kuuza madawa ya kulevya, Sometimes wanasema nimefungwa, sometimes nimenyongwa, sometimes nimekamatwa hususan pindi ninaposafiri kwenda nchi mbalimbali, na sasa hivi nimeambiwa kwamba natumia madawa ya kulevya, Well, ni habari ambazo mheshimiwa mkuu wa mkoa amesema hana uthibitisho nazo lakini amelazimu kutaja majina kadha wa kadha ambayo ndio hivyo ameyataja mengine kwenye vyombo vya habari, na ameamuru twende tukaripoti kesho (leo Feb 3), ifikapo saa tano asubuhi,”>>>Mi nasema hivi, nitaenda, nitaripoti, kwasababu ni wito ambao ametaja mkuu wa mkoa wangu kuona amefanya, unaambiwa kubali wito, usikatae neno. Kwahiyo tutaenda kesho, na ntamsikiliza yale ambayo anataka kuniambia, iwapo tukishajua which is true, which is not, then tutajua from there what to do, sasa hivi sina cha kusema, sina cha kufanya, because bado sijaonana naye, kwa sasa niacheni tu nirelat but I want to assure you one thing, I am not a drug addict, and I am not a drug abuser, and if I was nadhani we all know how drug addicts act, we all know how drug abusers wanakuwaga. I want you guys to relax, do not worry, everything is going to be fine.”
Download App ya Wema kwenye #Bio yake ya Instagram Instagram.Com/WemaSepetu.
Maneno makali ya Wema Sepetu matumizi na uuzaji wa dawa za kulevya…
Reviewed by Unknown
on
09:12:00
Rating:
Hakuna maoni: