JINSI WANAWAKE WALIOTELEKEZWA WALIVYOGEUKA "DILI' KWA MAKONDA

Unaweza kusema mgeni njoo mwenyeji apone. Ndivyo inavyotokea muda huu nje ya ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kuibuka kwa wafanyabiashara wanaowauzia chai na vitafunwa wanawake wenye watoto ‘waliotelekezwa’ na waume zao.


Wanawake hao tangu juzi wamekuwa wakiripoti katika ofisi hizo kupata msaada wa kisheria baada ya kutelekezwa na waume zao.

Leo Jumatano Aprili 11, 2018 MCL Digital imepiga kambi kuanzia saa 12 asubuhi na kushuhudia wafanyabiashara hao ndogondogo wakiwauzia chai na vitafunwa wanawake waliofika katika ofisi hizo.

Wanawake kwa vijana waliobeba chupa za chai na uji walionekana kuhudumia eneo hilo huku wengine wakiwa na ndoo za vitafunwa.

Wenye watoto walihangaika kuwapatia chochote wakati wakisubiri wanasheria wa walioandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa waanze kuwasikiliza.

Mmoja wa wafanyabiashara Salim Juma amesema zoezi hilo limeleta neema kwao.

"Tulikuwa tunazunguka mtaani kutafuta wateja ila ndani ya siku mbili hizi mambo mazuri mzigo unaisha hapa hapa," amesema Salim anayeuza vitumbua
JINSI WANAWAKE WALIOTELEKEZWA WALIVYOGEUKA "DILI' KWA MAKONDA JINSI WANAWAKE WALIOTELEKEZWA WALIVYOGEUKA "DILI' KWA MAKONDA Reviewed by Unknown on 04:35:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.