Clinton na Trump wapigania majimbo muhimu
Hillary Clinton na Donald Trump wamezidisha kampeni zao, hasa kwenye majimbo yanayoshindaniwa sana, huku kura za maoni zikionesha wamekaribiana sana zikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi mkuu.
Wawili hao kwa mara nyingine wameshambuliana kwenye mikutano ya kampeni, kila mmoja akisema mwenzake hawezi kuongoza.
Bi Clinton, ambaye uongozi wake kwenye kura za maoni kitaifa unaonekana kufutika siku za karibuni, amesema mpinzani wake wa chama cha Republican hawezi kudhibiti hisia zake na ana mtazamo hasi dhidi ya wanawake.
Bw Trump naye amesema Bi Clinton ataandamwa na uchunguzi wa jinai hadi ikulu ya White House.
Mgombea huo anaonekana kuimarika dhidi ya Bi Clinton katika majimbo yanayoshindaniwa, kwa mujibu wa kura za maoni.
Alhamisi, mkewe Melania alijitokeza kwenye mkutano wa kampeni kumtetea.
Kwenye hotuba yake ya kwanza tangu Julai wakati wa mkutano wa kitaifa wa chama cha Republican, mwanamitindo huyo wa zamani alizungumzia maisha yake kama mhamiaji na akasema mumewe ataifanya Marekani kuwa nchi ya haki.
Bill Clinton ataitwa nani Hillary akishinda?
George HW Bush kumpigia kura Clinton
Clinton atabahatika mara ya pili?
Aidha, ameapa kuongoza kampeni dhidi ya watu kudhalilishwa na kudhulumiwa kwenye mitandao iwapo atakuwa mama wa taifa.
Akiongea kwenye viunga vya mji wa Philadelphia amesema atakabiliana na utamaduni ambao "umekuwa kaidi sana na katili".
Hata hivyo, hakuzungumzia tabia ya mumewe ya kuwashambulia na kuwatusi wapinzani wake kwenye mitandao ya kijamii.
Bw Trump ameimarika dhidi ya Bi Clinton katika majimbo kadha ya kushindaniwa, yakiwemo majimbo ya Florida na North Carolina, kwa mujibu wa kura za maoni.
Obama: Mustakabali wa dunia utakuwa kwenye mizani
Kila unachohitaji kujua kuhusu uchaguzi Marekani
Baadhi ya kura za maoni za kitaifa zinaonesha wawili hao wana kiwango sawa cha uungwaji mkono
Makadirio ya utafiti wa Reuters/Ipsos yanaonyesha uwezekano wa Bi Clinton kushinda kura za wajumbe 270 zinazohitajika kushinda Jumanne kwa sasa ni 90% chini kutoka 95%.
Bw Trump ndiye anayeonekana kuimarika zaidi, na alifanyia hilo mzaha wikendi ya mwisho inapowadia.
Ametumia habari za FBI kuanzisha uchunguzi mpya kuhusu barua pepe za Bi Clinto kumshambulia zaidi mpinzani wake.
"Ndio hao Wanaclinton tena - mwakumbuka vikao vya kumuondoa rais madarakani na matatizo mengine," Bw Trump aliambia waliohudhuria mkutano Jacksonville, Florida.
"Haya siyo mtayotaka, jameni. Twahitaji mtu aliye tayari kfuanya kazi."
Baadaye mkutano wa usiku Carolina Kaskazini, akizungumzia masuala ya ulinzi, alisema hawezi kutafakari Bi Clinton akiwa amiri jeshi mkuu.
Bi Clinton ameendelea kuangazia sifa za Bw Trump, na alisema CDunia
na Kaskazini: "Ametumia muda wake wote wa kampeni akiwapa filimbi wafuasi wake wenye chuki.
"Hili halijawahi kufanyika kwa mgombea wa chama kikubwa."Aliongeza: "Iwapo Donald Trump atashinda uchaguzi tutakuwa na amiri jeshi mkuu ambaye hajielewi na ambaye mawazo yake ni hatari."
Rais Barack Obama amekuwa akitia bidii kumfanyia kampeni Bi Clinton, akijaribu kuwashawishi wapiga kura vijana na Wamarekani weusi wampigie kura.
Utathmini wa kura za mapema unaonesha huenda wapiga kura weusi hawajitokezi kwa wingi kupiga kura kama walivyofanya kumpigia kura Obama mwaka 2012.
Trump: Clinton ataanzisha Vita Vikuu vya Dunia
Bi Clinton alipata nguvu zaidi pale mpinzani wake mkuu wa wakati wa mchujo Bernie Sanders alipojitokeza mkutano wake wa kampeni.
Kwenye mkutano huo Carolina Kaskazini Alhamisi jioni Bw Sanders alimsifu Bi Clinton kwa kujitolea kuinua ujira wa chini na kuangazia ukosefu wa usawa.
Nyota wa muziki Pharrell Williams pia alihudhuria na kumsifu Bi Clinton kwa kutetea haki za wanawake
Clinton na Trump wapigania majimbo muhimu
Reviewed by Unknown
on
09:59:00
Rating:
Hakuna maoni: