DADA YAKE DIAMOND PLATNUMZ "ESMA" YAMTOKA MAPOVU KUHUSU ANAYEJIITA BABA YAKE DIAMOND
Dada wa msanii Diamond platnuz Esma Platnumz amesema hakuwahi kumtabiria wala kutegemea kuwa kaka yake Diamond angekuja kuwa mtu maarufu kimataifa japo alikuwa akionesha kupenda muziki tangu akiwa mdogo.
Hata hivyo Esma amesema maswala yanayoandikwa kwenye magazeti kuhusiana na Baba yake siyo ya kweli kwa kuwa yeye anamfahamu baba yake mzazi na mtu aliyejitokeza kwenye magazeti siyo baba yake na hamfaham kabisa.
Pia Esma hakusita kuongelea taarifa zilizozagaa kwamba mama Daimond hana mahusiano mazuri na wifi yao Zari na kusema hawana tatizo lolote na wifi yao na hakuna mzazi asiye furahia wajukuu hivyo watu wanayoyaona katika magazeti siyo ya kweli na wasiyatilie mkazo, huku akimalizia kwa kusema kuwa anampenda mume wake Petit Man.
DADA YAKE DIAMOND PLATNUMZ "ESMA" YAMTOKA MAPOVU KUHUSU ANAYEJIITA BABA YAKE DIAMOND
Reviewed by Unknown
on
10:05:00
Rating:
Hakuna maoni: