Akothee azungumzia ushindi wa Afrimma ‘ndio kwanza nimeanza’



Mwaka huu Akothee amefanikiwa kuwatoa kimasomaso wasanii wa kike nchini Kenya kwa kuitwaa tuzo ya msanii bora wa kike Afrika Mashariki ya Afrimma zilizofanyika wiki iliyopita jijini Dallas, Marekani.
720296cf-a546-468e-960f-b02c8be1b587
Kwake, tuzo hiyo imedhihirisha kuwa uwekezaji alioufanya kwenye kazi zake haujaenda bure. Katika kipindi cha mwaka mmoja tu, Akothee amefanikiwa kutengeneza nyimbo zilizofanya vizuri barani akiwashirikisha nguli wa Afrika, Diamond kwenye Sweety Love ambayo hadi sasa ina views zaidi ya milioni 2.9 na Flavour kwenye Give It To Me yenye views zaidi ya milioni 1.5 kwenye Youtube.
c76f7f8f-0222-4a06-b060-c4eeb15620ba
Wimbo Yuko Moyoni uliotoka miezi mitatu iliyopita nao unafanya vizuri.
Nyimbo hizo zimemfanya kuwa msanii wa kike wa Kenya mwenye video zilizotazamwa zaidi huku akielekea kuanza kula sahani moja na kundi la Sauti Sol kwa kutengeneza video zinazopata umaarufu mtandaoni.
43105b48-1380-4dbc-882d-9eedecc5f760
Akiongea na Bongo5 kuhusu ushindi wa Afrimma, Akothee amesema mashabiki wake ndio waliomwezesha. “Nimehisi support kubwa kutoka kwa mafans wangu na nimeelewa ya kwamba kazi yangu ya muziki wameipenda na kuniaminia,” anasema.
“Tuzo hii ina maana ya kwamba ndio mwanzo wa mbio sasa, manaake kimeeleweka sasa nitie bidii ili ku-maintain position na kwenda juu zaidi. Tuzo yaonyesha ya kwamba nimeenda kiwango cha international,” ameongeza.
Muimbaji huyo amedai kuwa mashabiki wake wajiandae na kazi mpya mwezi ujao.
5e82b608-b3c5-4638-85da-919c80dc35af
“Nina mengi ya kuwapa kuanzia mwisho wa November nitawapa vitu vizito. Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa kuchukua fursa Yao kunisupport.”
Jumamosi hii Akothee atatumbuiza kwenye African Entertainment Awards USA huko New Jersey, Marekani
Akothee azungumzia ushindi wa Afrimma ‘ndio kwanza nimeanza’ Akothee azungumzia ushindi wa Afrimma ‘ndio kwanza nimeanza’ Reviewed by Unknown on 07:17:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.