Katika Maisha Hakuna Anayejua Kitatokea Nini Siwezi Kumsema Vibaya Vanessa- Jux

Katika Maisha Hakuna Anayejua Kitatokea Nini Siwezi Kumsema Vibaya Vanessa- Jux
Mkali wa muziki wa RnB Bongo, Jux amesema ingawa wameachana na Vanessa Mdee siyo sababu ya kumsema vibaya.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Utaniua’ ameiambia E-Newz ya EATV kuwa analazimika kuwa na nidhamu hiyo kwa sababu kwenye maisha kuna leo na kesho.

“Unajua katika maisha hakuna anayejua kesho kutatokea nini, mimi siwezi kutoa kauli yoyote kwa sababu Vanessa bado nampenda. Tumefanya vitu vingi sana, nampenda na nitaendelea kumpenda kwa kushirikiana kwenye mambo mengi,” amesema Jux.

Katika hatua nyingine alipoulizwa iwapo Vanessa atamfuata na kumtaka warudiane kama atakuwa tayari, Jux alijibu;

“Siwezi nikaliongelea hilo, sijajua kwa hiyo moment itakuwaje, mimi naishi pia siwezi jua kesho nitakutana na nani kitatokea nini, huwezi jua yeye atakutana na nani kitatokea nini, so siwezi nikatoa hilo jibu sasa hivi lakini tuone itakavyokuwa, tunaendelea kuishi you never know,” amesema.

Kipindi cha mapenzi yao waliweza kutoa wimbo wa pamoja uitwao Juu, pia walishirikishwa katika wimbo wa Nikki wa Pili ‘Safari’
Katika Maisha Hakuna Anayejua Kitatokea Nini Siwezi Kumsema Vibaya Vanessa- Jux Katika Maisha Hakuna Anayejua Kitatokea Nini Siwezi Kumsema Vibaya Vanessa- Jux Reviewed by Unknown on 05:52:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.