PETER Msechu Aponzwa na Kauli ‘Nafumaniwa Kila Siku Mtaani Kwetu’


Muimbaji Peter Msechu alijikuta matatizoni wiki iliyopita baada ya kutoa kauli ya mzaha kwamba yeye ni mtu anayefumaniwa kila siku mtaani kwake.

Msechu amedai muda mchache baada ya kauli hiyo kusambaa mke wake alianza kupigiwa simu na watu mbalimbali kitu ambacho kilimfanya achanganyikiwe.

Kauli hiyo aliitoa Msechu baada ya kuulizwa swali na kituo kimoja cha redio kwamba wasichana wengi hawapendi kutoka kimapenzi na wanaume wenye vitambi ndipo muimbaji huyo akajibu mbona yeye mtaani kwake wasichana wengi wanamgombania huku akidhihaki tena ameshikwa ugoni mara kadhaa.

Akiongea Jumatano hii katika kipindi cha Yaliyomoyamo cha Redio One Stereo, Msechu amedai kauli hiyo aliitoa kwa mzaha na baadhi ya watu walishindwa kuielewa.

“Yaani baada ya ile kauli kusambaa hawakunitafuta mimi wala media, wakatafuta mzazi wangu, nilikwambia mwanao mwambie aache muziki sasa angalia anafumaniwa kila siku. Mke wangu akajazwa maneno ametoka ofisini amedata,” alisema Msechu.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Yakawa’ amedai muziki kwa sasa unawafanya wasanii kubadilisha aina ya muziki waliokuwa wanafanya awali na kuingia kwenye muziki wa kutegemea kiki.
PETER Msechu Aponzwa na Kauli ‘Nafumaniwa Kila Siku Mtaani Kwetu’ PETER Msechu Aponzwa na Kauli ‘Nafumaniwa Kila Siku Mtaani Kwetu’ Reviewed by Unknown on 20:58:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.