MCHEKESHAJI EBITOKE ADAI AMEKUBALIWA NA BEN POL
Msanii wa vichekesho Anastazia Kisaveli alimaarufu kama Ebitoke ameweka wazi jambo ambalo anavutiwa zaidi na Ben Pol na kusema ni vile msanii huyo alivyompenda na kumkubali jinsi alivyo.
Ebitoke ambaye inadaiwa anatoka kimapenzi na Ben Pol amesema hayo kudai Ben Pol hakumtenga wala kumdharau kutokana na kazi yake hiyo bali alimkubali na kumuhakikishia kumpa support katika kazi yake hiyo ili afanikiwe zaidi na zaidi.
"Kuna watu wananitisha kweli wanakuja 'DM' wengine wananitukana, wengine hivi wewe Ebitoke unaweza kuwa na Ben Pol? Hivi mimi wananionaje hawa watu wasinichukulie poa poa. Tunachotarajia sasa Ben Pol kwanza lazima anipe 'support' kwa kila kitu nachokifanya na mimi lazima nihakikishe natimiza malengo yangu kwa sababu amesema atanisapoti kuanzia kazi yangu nayofanya mpaka mbeleni kwa hiyo huyo ni mwanaume wa kweli kwangu, ambaye amekubali kazi yangu nayofanya, amenikubali jinsi nilivyo hajanibagua nimefurahi sana aliposema kuwa lazima anipe nguvu kutumiza malengo yangu" alisema Ebitoke
Mbali na hilo Ebitoke anasema kuna mambo mengi yeye na Ben Pol wameyapanga na anaamini kuwa yatatimia mbele ya safari katika maisha yao ya kila siku, ila anasema kaka zake yeye walimjia juu kuona hizo stori za mahusiano na Ben Pol lakini baadaye walielewa kuwa anachofanya ni kutafuta maisha hivyo ilibidi wamuache na kazi yake hiyo ya uigizaji na kuendelea kumpa 'Support'
MCHEKESHAJI EBITOKE ADAI AMEKUBALIWA NA BEN POL
Reviewed by Unknown
on
22:27:00
Rating:
Hakuna maoni: