Haya Hapa Mahojiano ya HAMISA Mobeto Kuhusu Mtoto wa Diamond....
..
Tangu ilipoachiwa video ya ‘Salome’ ya mkali wa Bongofleva Diamond Platumz akishirikiana na Rayvanny, kulianza maneno kuwa Diamond anatoka kimapenzi na mwanamitindo Hamisa Mobeto.
Hamisa alikuwa mmoja wa warembo walioonekana kwenye video hiyo. Wiki kadhaa mbele, Hamisa alionekana kuwa na ujauzito na hapo ndipo maneno yalipozidi kwenda mbali zaidi kwamba mhusika wa mimba hiyo ni mwanamuziki Diamond.
Yafuatayo ni mazungumzo kati ya muandishi wa habari na bibie Hamisa Mobeto kuhusu suala hilo:
Hamisa alisema kuwa ni kweli amesekia maneno mengi kuhusu mimba yake akihusishwa mwanamuziki Diamond kama inavyosemwa.
“Huu uvumi unataka niweke wazi maisha yangu. Hilo halitajitokeza kwangu kwani mtu akishaumwa na nyoka akimuona mjusi anamuogopa. Baba wa mtoto wangu mtarajiwa namjua mimi na familia yangu. Nadhani inatosha.
“Sidhani kama ni lazima nimtaje kwenye media (vyombo vya habari) lakini wale wanaosema ni Diamond tafadhali sana, siye. Baba wa mtoto wangu yupo na sio matangazo ya biashara kila mtu majue mpenzi wangu.
“Hao wanaotutukana mbona maisha yao wameyaweka siri, au mimi tu ndiyo nijianike? Siwezi kufanya hivyo, najua nachokonolewa ili niseme lakini sitasema,” amesema Hamisa.
Amesema kuwa kwa sasa yeye ni mtu mpya na kwamba mashabiki wake watamjua kwa kazi zake na siyo maisha yake binafsi kwa sababu ameshajua madhara ya maisha yake hadharani.
“Maisha yangu binafsi yatabaki kuwa yangu mimi mwenyewe ila ya kibiashara yatajulikana na kila mtu. Mimi kwa sasa sihitaji sifa za kijinga, nahitaji mashabiki zangu wafahamu nafanya nini katika jamii na wanishabikie hivyo, sio kwa maisha yangu binafsi,” amesema.
“Kuruhusu ushabiki katika maisha yako binafsi hasa ya mapenzi ni kujijengea uadui na marafiki wa uongo ambao wengi wao wanakuja kinafiki na kujifanya wanakufahamu kiundani au mpenzi wako kumbe ni waongo. Wanataka kuwavuruga na wakifanikiwa hutawaona,” alisema.
HT @ MTANZANIA

Reviewed by Unknown
on
00:21:00
Rating: 5
Hakuna maoni: