MASKINI..Chid Benz Amtoa Chozi Mama Yake
MKALI wa michano, Rashid Mwakwiro ‘Chid Benz’ amemtoa machozi mama yake baada ya kuachia ngoma yake mpya ya Muda alioshirikiana na mkali mwenzake, Aboubakar Katwila ‘Q Chillah’.
Akizungumza na Over Ze Weekend, Chid aliyekuwa amepotea kwenye gemu baada ya kuzama kwenye matumizi ya dawa za kulevya alisema, tangu aachie ngoma hiyo akiwa kwenye interview mbalimbali mama yake amekuwa akimpigia simu mara kwa mara na kusema kuwa moyo wake hautulii unapiga sana arudi nyumbani.
“Wengi wameupokea wimbo huu kwa hisia sana. Watu wanatuma meseji na kusema wametokwa na machozi. Mama mara kwa mara amekuwa akinipigia simu na kuniambia fanya urudi mapema uwe nyumbani tu nalia sana. Shangazi zangu, mamdogo, mabibi na marafiki zangu wananipigia wananiambia wanalia sana baada ya kuusikia wimbo huu,” alisema Chid.
Akiongelea kuhusiana na matumizi ya madawa ya kulevya aliyopitia, Chid alisema alikuwa akitumia unga kwa kiwango kikubwa sana;
“Nimevuta sana na wote mliona picha na video. Kile kitu ni kibaya lakini nilikuwa natumia kwa siku laki 4, 5, 6 hadi saba. Nikiishiwa nafikiria nani nimpigie simu nimuombe hela. Kila siku lazima nilale hoteli tena Kinondoni, kila siku lazima nilipie kuanzia 50,60 kwa siku nafanya. Kila siku lazima nivute ndiyo niweze kuongea kwa hiyo hela nilikuwa napata kupitia simu tu, kila ninayempigia ananisikitikia na kunitumia,” alimaliza Chid Benz ambaye kwa sasa ameachana na matumizi hayo na kujikita kwenye muziki.
MASKINI..Chid Benz Amtoa Chozi Mama Yake
Reviewed by Unknown
on
04:43:00
Rating:
Hakuna maoni: