Diamond: Nlipigiwa simu na Psquare pamoja na Fally Ipupa kuhusu ishu ya Zari
nasseb Abdul maarufu kama Diamond Platnum amefunguka juu ya post ya Instagram aliyoiandika wiki chache zilizopita na baadae kuifuta baada ya picha ya mzazi mwenza Zari akiogelea na mwanaume mwingine.
Muimbaji huyo amedai baada ya tukio hilo kutokea, alipigiwa simu na mastaa mbalimbali kutaka kujua nini kimetokea.
“Baada ya post yangu ya insta wasanii wengi walinipigia simu, Psquare na Fally Ipupa walinicheki kutaka kujua nini kimenikuta,” alisema Diamond.
Diamond amesema baada ya kupost picha pamoja na ujumbe ambao haukuwa mzuri kwa Zari, mrembo huyo wa bosi wa WCB alionyesha kutofurahishwa na ujumbe huo.
“Baada ya Zari kuona post yangu Insta alikuwa ofisini na alirudi nyumbani na aliponielewesha nilikuwa mpole na nikamuelewa,” alisema Diamond.
Hata hivyo shemeji yake ambaye ni binamu wa marehemu Ivan, alikanusha tuhuma za kutoka na mrembo na kusema hawezi kufanya hivyo na kwani anamuheshimu
Diamond: Nlipigiwa simu na Psquare pamoja na Fally Ipupa kuhusu ishu ya Zari
Reviewed by Unknown
on
21:24:00
Rating:
Hakuna maoni: