Saida Karoli: Diamond na Belle 9 waliniokoa nisirudi kijijini
Licha ya kuwa mpambanaji kwa muda mrefu ili arudi tena kwenye muziki, kumbe Saida Karoli alishakata tamaa ya kutoboa tena.
Mama huyo mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni amedai kuwa baada ya Belle 9 na Diamond kuachia nyimbo zao walizotumia baadhi ya vitu kutoka kwenye wimbo wake wa ‘Maria ya Salome’ ndio zilimpa nguvu mpya ya kurudi kwenye muziki.
Mbali na hilo tena alishaanza safari ya kwenda kuanza maisha mapya kijijini.
“Nilishatamani kuacha muziki na nilishawahi kuhamisha baadhi ya vitu vyangu kurudi kijijini na ndiyo kipindi hiko hiko Belle Nine na Diamond walitoa nyimbo ya Chambua kama karanga, wakanirudisha maana ilikuwa safari kabisa,” amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii.
Saida Karoli: Diamond na Belle 9 waliniokoa nisirudi kijijini
Reviewed by Unknown
on
05:40:00
Rating:
Hakuna maoni: