Jide Afunguka Haya baada ya Kuachwa na Mnigeria Wake
Jide afunguka ya kuachwa na Mnigeria wake
Wakati maneno ya chini chini yakiwa yanaendelea kuhusu kupigwa kibuti na mpenzi wake mpya Spicy kutoka Nigeria, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ amefunguka na kusema wabongo wengi wanapenda wenzao waharibikiwe na kuwataka kuacha kuwaziana mabaya.
Jide amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya maneno kuzagaa kuwa amepigana kibuti na Mnigeria huyo ikiwa ni siku wiki chache baada ya kuandika maneno yaliyomo kwenye wimbo wa Rosella katika mtandao wa Instagram.
“Niko vizuri na Spicy, yale maneno niliandika kwa ajili ya muziki, watu wanapenda kuona wenzao wanaharibikiwa, kwanini wanakimbilia kuamini nina matatizo na Spicy na hawafikirii kuhusu kazi yangu? Niwakaribishe waje kwenye show yangu ya uzinduzi pale Lugalo Uwanja wa Gofu Ijumaa hii,” alisema Jide.
Lady Jaydee anayetamba na wimbo wa Rosella alioshirikiana na h_art the band kutoka Kenya anatarajiwa kuzindua albamu yake ya saba tarehe 31 ya mwezi huu.

Reviewed by Unknown
on
05:32:00
Rating:
Hakuna maoni: