Je wajua?....Vijana 29 Huambukizwa UKIMWI Kila Saa Moja

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linasema vijana 29 huambukizwa virusi vya ukimwi, VVU kila saa moja.

Katika ripoti yake mpya iliyotolewa leo, UNICEF inasema maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa vijana yanakadiriwa kuongezeka kutoka 250,000 mwaka 2015 hadi kufikia 400,000 ifikapo mwaka 2030.

Ripoti hiyo inapendekeza mikakati ya kuongeza kasi katika kuzuia VVU miongoni mwa vijana na kutibu wale ambao tayari wameambukizwa kama vile kuwekeza katika uvumbuzi ikiwemo wa kitaifa, kuimarisha ukusanyaji wa takwimu, kutokomeza ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia na elimu kwa vijana.

Wakati huo huo, kumefanyika kongamano la kimataifa jijini Durban, Afrika Kusini kuhusu Ukimwi ambalo limewaleta pamoja UNICEF, wanaharakati na vijana kutoka kutoka sehemu mbalimbali Afrika kupata maoni yao.

UNICEF inasema mbali na mafanikio mengi yaliyopatikana, ufadhili wa fedha kwa ajili ya kukabiliana na Ukimwi umepungua tangu mwaka 2014.
Je wajua?....Vijana 29 Huambukizwa UKIMWI Kila Saa Moja Je wajua?....Vijana 29 Huambukizwa UKIMWI Kila Saa Moja Reviewed by Unknown on 06:30:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.