JK: “Tukiwekeza kwenye michezo, Tanzania itaandikwa kwa wino wa dhahabu”
wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema Tanzania ikiwekeza katika michezo hasa kuibua vipaji vya watoto inaweza ikapata wachezaji wazuri hapo baadae watakao itangaza nchi kimataifa.
Kikwete ameyasema hayo katika fainali za mpira wa kikapu kwa vijana zilizofanyika katika Kituo cha Vijana cha Michezo cha Jakaya .M. Kikwete jijini Dar es Salaam.
” Uwekezaji wa watoto wadogo kimichezo ni vizuri sababu unainua vipaji vya watoto na hatimaye kupata wachezaji wazuri hapo baadae kama wa mpira wa miguu, kikapu na wa pete. Kituo hiki kimefundisha zaidi ya watoto elfu hamsini,” alisema na kuongeza.
“Wakiwekeza hapa Tanzania itaandikwa kwa wino wa dhahabu miaka ijayo kupitia michezo ambao wachezaji wake watatoka katika kituo hiki.”
Aidha, Kikwete ameishukuru NBA Afrika kwa kuandaa mashindano hayo.
“Naishukuru NBA Afrika kwa uwekezaji walioufanya pamoja na kutuletea wataalamu na wakufunzi kuwafundisha na kuwapa maarifa watoto, sababu wamepata fursa kimichezo hasa mpira wa kikapu,” alisema.
JK: “Tukiwekeza kwenye michezo, Tanzania itaandikwa kwa wino wa dhahabu”
Reviewed by Unknown
on
22:16:00
Rating:
Hakuna maoni: