RAIS UHURU AHAIRISHA ZIARA YAKE NCHINI ANGOLA KUFUATIA MASHAMBULIZI KATIKA MJI WA MANDERA
RAIS Uhuru Kenyatta amesitisha ziara yake nchini Angola ili kuungana na familia na marafiki wa watu 12 waliouawa na magaidi katika Kaunti ya Mandera.
Msemaji wa Ikulu Bw Manoah Esipisu. Picha/PSCU
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Rais Kenyatta aliahidi familia zilizoathiriwa kuwa serikali itafanya juhudi zote kuhakikisha kwamba waliohusika wamekabiliwa kisheria.
“Rais Kenyatta amemtaka Naibu Rais William Ruto, amwakilishe jijini Luanda katika mkutano huo,” Msemaji wa Ikulu Manoah Esipisu alisema katika taarifa yake.
Rais alituma risala zake za rambirambi na kuwatakia waliojeruhiwa nafuu ya haraka.
“Kila Mkenya, awe Mwislamu au Mkristo anafahamu kuwa ni makosa kuua mtu asiyekuwa na hatia. Wakenya hawatakubali kugawanywa kwa misingi ya kidini, kwa kuwa hayo ndio madhumuni ya magaidi,” alisema rais.
Ugaidi
Rais aliwataka Wakenya wote waunge mkono juhudi za serikali kukabili visa vya ugaidi kote nchini.
“Ili tushinde vita hivi, sharti tuwe kitu kimoja. Njia moja ya kuonyesha umoja huo ni kushirikiana na maafisa wetu wa usalama wanapojitahidi kutulinda,” akasema.
RAIS UHURU AHAIRISHA ZIARA YAKE NCHINI ANGOLA KUFUATIA MASHAMBULIZI KATIKA MJI WA MANDERA
Reviewed by Unknown
on
06:35:00
Rating:
Hakuna maoni: