PICHA: Mrithi wa kocha Hans van Pluijm wa Yanga kawasili Dar es Salaam
Siku 14 baada ya Dar es Salaam Young Africans kupitia kwa kaimu katibu mkuu wake Baraka Deusdedit atangaze kukanusha klabu hiyo kuwa na mpango wa kumfuta kazi Hans van Pluijm na kurithiwa na kocha wa Zesco United ya Zambia George Lwandamina, hatimae leo October 24 ukweli wa taarifa hizo umeanza kufahamika.
Yanga walikanusha kuwa katika mpango wa kumfuta kazi kocha Hans van Pluijm October 10 2016 lakini sasa kuwasili kwa kocha mzambia mchana wa October 23 George Lwandamina Dar es Salaam kunaanza maliza uvumi wa tetesi hizo, Lwandamina tayari yupo Dar es Salaam licha ya kuwa Yanga hawajathibitisha lolote.
Kwa tetesi na habari zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zinaeleza kuwa kocha Lwandamina alishamalizana na Yanga na amesaini mkataba wa miaka miwili ya kumrithi kocha Hans van Pluijm.
PICHA: Mrithi wa kocha Hans van Pluijm wa Yanga kawasili Dar es Salaam
Reviewed by Unknown
on
03:14:00
Rating:
Hakuna maoni: