Mkutano wa Yanga wapigwa ‘stop’ na Mahakama, ni baada ya wanachama kuupinga mkutano huo
Baada ya masaa machache hapo jana Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji kuwaomba wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa dharura uliopangwa kufanyika tarehe 23-10-2016, taarifa zilizoenea ni kwamba, mahakama imezuia mkutano huo kufatia baadhi ya wanachama kwenda mahakamani kufungua kesi kupinga mkutano huo wa dharura.
Mmoja wa wanachama hao ni Frank Chacha ambaye amethibitisha kufungua kesi hiyo, akizungumza kupitia Radio One stereo ya jijini Dar es Salaam, Chacha amesema mkutano wa kwanza ulikuwa unamakosa na mkutano wa pili pia umeitishwa kwa makosa na mkataba umeshasainiwa na wakati huu sio wa kwenda kuujadili.
“Ni Kweli mkutano ulikuwa umepangwa kuganyika tarehe 23-10-2016 ambapo agenda zaidi ya 13 zingepaswa kujadiliwa kinaga ubaga, lakini hadi tunavyozungumza leo hii (October 21) tumeiomba mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuahirisha huo mkutno.”
“Tumefanikiwa kufungua kesi namba 293 (2016) kesi ndogo namba 214 (2016) kati ya Frank Chacha muombaji wa kwanza na Magoma mwombaji wa pili, walalamikiwa ni Bodi ya Udhamini ya klabu ya Yanga na kampuni ya Yanga Yetu.”
“Katika maombi yetu ya dharura tumeomba mambo yafuatayo, Mkutano wa tarehe 23-10-2016 uzuiliwe kwasababu ni mkutano batili haujafata taratibu za kisheria kwasababu notice imekuja nje ya utaratibu pia makabrasha yalitakiwa yatolewe siku sba kabla ya mkutano kitu ambacho hakijafanyika, notice siku 30 kabla ya mkutano kitu ambacho hakikufanyika.”
“Pia tumeomba kusitishwa utekelezaji wa mkataba kati ya Yanga Yetu na Bodi ya wadhamini uliosainiwa mnamo tarehe 03-10-2016. Mahakama sikivu tukufu mbele ya mheshimiwa Mwambapa, imetoa order hizo kuzuia mara moja mkutano usifanyike na tayarumeshari tumeshaipa taarifa Bodi ya wadhamini na klabu ya Yanga mkutano huo usifanyike na mabango mengine kuhusiana na order hiyo tayari yameshabandikwa kwenye uwanja wa Kaunda.”
“Kwa kifupi, hakuna mkutano tena kwa mujibu wa order ya mahakama.”
Source: Shaffih Dauda

Reviewed by Unknown
on
01:30:00
Rating:
Hakuna maoni: