Nitatoa mahari ya Madee asema Tunda Man

Msanii wa bongo fleva Tunda Man amemshauri rafiki yake Madee kufunga ndoa kwa kuwa amemzidi umri na ana mwanamke ambaye anampenda hivyo haoni sababu ya Madee kuacha kufunga ndoa na yupo tayari kuchangia mahari ya Madee.
Akiongea na #Sammisago Kwenye #ENews Tunda amewapongeza wasanii wezake waliofunga ndoa akiwemo Nyandu ToziMwana Fa , Mabeste na wengine Tunda amewasihi wasanii wenzie wa dini ya kiislamu kufunga ndoa kwa kuwa zitawasaidia kuongeza heshima katika jamii inayowazunguka.
Hata hivyo Tunda amewachana wasanii wanaoongopa kufunga ndoa wakihofia kushuka kwa muziki wao kwamba hawana hofu ya Mungu kwani kupanda na kushuka ni mipango ya Mungu na wapo kina Mr. Blue wamefunga ndoa na bado wanafanya vizuri kimuziki.
Nitatoa mahari ya Madee asema Tunda Man Nitatoa mahari ya Madee asema Tunda Man Reviewed by Unknown on 10:03:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.