Historia Fupi ya Mlinzi wa Mbunge Aliyeshinda Ubunge Kenya
Aliyekuwa Afisa wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, Nimrod Mbithuka alipofika katika Bunge Kenya mwaka 1998 alipewa jukumu la kumlinda Waziri Francis Nyenze.
Nyenze alikuwa ameibuka mshindi katika kiti cha ubunge katika jimbo la Kitui Magharibi na ndipo aliteuliwa kuwa waziri na hivyo kupewa mlinzi atakayehakikisha usalama wake.
Siyo yeye tu aliyekuwa amepewa jukumu hilo la ulinzi, bali pia polisi wengine walipewa wabunge wakuwalinda ambapo kazi yake kila siku ilikuwa kuhakikisha usalama wa Waziri Nyenze alipokuwa akitoka nyumbani kwenda bungeni au kwenye shughuli nyingine.
Mbai alikuwa mlinzi wa mbunge huyo kwa miaka minne (1998-2002). Baada ya Waziri Nyenze kushindwa kutetea kiti chake mwaka 2002, Mbai aliteuliwa kuwa mlinzi wa Dr Alfred Mutua aliyekuwa ameteuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali.
Aliifanya kazi hiyo kwa miaka 10 kabla ya kungatuka na kwenda kugombea nafasi ya Ugavana katika Kaunti ya Machakos kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Mwaka 2013, Mbai alijiuzulu kutoka katika utumishi wa jeshi la polisi, na hivyo kuteuliwa na Dr Mutua katika nafasi ya ngazi ya juu kwenye uongozi wa Kaunti.
Katika uchaguzi wa ubunge uliofanyika Agosti 8 mwaka huu, Mbai aliibuka na ushindi katika eneo hilo lililotawaliwa na Chama cha Narc akimshinda mbunge wa sasa wa eneo hilo, Meja Mstaafu Marcus Mutua Muluvi.
Katika uchaguzi huo, Mbai ambaye ni Mbunge Mteule wa Kitui Mashariki alijizolea kura 14,256 akimuacha mbali mpinzani wake Militonic Kitute aliyepata kura 10,899 akiwa ni mgombea wa Chama cha Narc huku Meja Muluvi wa Chama cha Wiper akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 5,436.
Wakati akifanya shughuli za kiutendaji katika ofisi ya Gavana Mutua ndipo alianza msingi wa kujikita zaidi katika siasa. Kabla ya hapo amewahi kufanya kazi kama afisa anayehusika na masuala ya ugatuzi, kilimo, mifugo na maendeleo ya uvuvi.
Wakati akisoma katika Shule ya Sekondari ya Wavulana iliyopo Kitui Kusini, walimu wengi walikuwa wakimsifia kwamba anaweza kuwa kiongozi kutokana na tabia walizoziona ndani yake.
Awali alikuwa mlinzi wa mtu, lakini kuanzia atakapoapishwa kuwa mbunge, mtu mwingine ataajiriwa kupepeleka kazini, kufungulia mlango wa gari kama sheria inavyoagiza na pia kama alivyofanya yeye kwa Waziri Nyenza na Msemaji wa Serikali, Dr Mutua.
Madaraka na upendeleo wanaopataiwa viongozi mbalimbali huenda vikawa ni sababu za kijana huyo aliyekua akichunga mbuzi katika eneo la Zombe, Kaunti ya Kitui enzi za utoto wake kujiunga katika siasa za ushindani
Historia Fupi ya Mlinzi wa Mbunge Aliyeshinda Ubunge Kenya
Reviewed by Unknown
on
00:18:00
Rating:
Hakuna maoni: