ONA HAPA MKUU WA WILAYA AKIJENGA MADARASA NA KUAGIZA WAZAZI WAZEMBE WAKAMATWE MARA MOJA,NI MGANDILWA WA KIGAMBONI....SOMA ZAIDI HAPA
Leo tarehe 3/11/2016 Mkuu Wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa amefanya ziara katika Kata ya Somangila ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Kata mbalimbali za Wilaya ya Kigamboni ili kushirikiana na wananchi katika shughuli za kimaendeleo, kusikiliza na kutatua kero zao moja kwa moja kwa kuwafuata wananchi walipo.
DC Mgandilwa alishirikiana na wananchi katika kujenga vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Mwongozo iliyopo Kata ya Somangila. Shuleni hapo DC ameweza kuchanganya ZEGE na baadae kuibeba akishirikiana na wazazi pamoja na mafundi ujenzi ambapo ujenzi wa msingi wa vyumba hivyo ulianza asubuhi na kukamilika mchana.
Katika mkutano wa hadhara baada ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, DC Mgandilwa ameagiza wazazi wa wanafunzi wote watoro ambao hawakuwepo leo shuleni Mwongozo kuwa wakamatwe na kuwekwa ndani kwani wazazi hao ni wazembe wameshindwa kuwajibika ili watoto wao wafike shuleni.
Amesisitiza wananchi kujitoa katika kushiriki shughuli za kimaendeleo na kuwa yeye yuko tiyari Muda wowote kushirikiana nao kufanya kazi pale watakapomtaarifu.
Ziara ya Mkuu wa wilaya inalenga kumpa fursa DC kushirikiana na wananchi katika shughuli za kimaendeleo, kusikiliza na kutatua kero zao moja kwa moja katika maeneo wanayoishi.
ONA HAPA MKUU WA WILAYA AKIJENGA MADARASA NA KUAGIZA WAZAZI WAZEMBE WAKAMATWE MARA MOJA,NI MGANDILWA WA KIGAMBONI....SOMA ZAIDI HAPA
Reviewed by Unknown
on
10:39:00
Rating:
Hakuna maoni: