Familia ya Prince yatoa kauli ya mwisho kuhusu Jay Z kununua haki za muziki wa Prince.
Familia ya Pop staa Prince aliyefariki mwaka huu imetoa kauli juu ya haki za muziki wa Prince kuuzwa ka kampuni ya Jay Z ya TIDAL kwa ada ya dola milioni 40.
Jay-Z alikutana na dada wa Prince “Tyka’ hivi karibuni kuongelea dili hili na dada huyo na mume wake walibidi wakaechini na familia nzima kuongelea jambo hili,
Familia ya Prince pia imekasirishwa na kitendo cha TIDAL kutengeneza na kutoa album 15 za Prince ili watu wazisikilize mtandaoni baada tu ya kifo chake.
Prince alisaini mkataba na TIDAL ya Jay Z mwaka 2015 na kutoa album yake ya HITnRUN Phase One,ila bado familia haijapata ushahidi kuwa Jay Z alimlipa Prince dola $750,000 kwa album hio.
Familia ya Prince yatoa kauli ya mwisho kuhusu Jay Z kununua haki za muziki wa Prince.
Reviewed by Unknown
on
11:09:00
Rating:
Hakuna maoni: