UJUMBE ALIOANDIKA EDWARD LOWASSA BAADA YA KUTIMIA MWAKA MMOJA TOKEA SIKU YA KUPIGA KURA
Tanzania imetimiza mwaka mmoja tangu ilipofanya uchaguzi wake mkuu ambapo watanzania walipata nafasi ya kupiga kura kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais wote wataoliongoza taifa kwa miaka mitano.
Uchaguzi Mkuu ulifanyika tarehe 25 Oktoba 2015 ambapo ulikuwa ni mmoja ya chaguzi zilizokuwa na ushindani mkubwa zaidi kuwahi kutokea Tanzania tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Ushindani mkubwa ulikwa kati ya wagombea wa Urais, Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akipeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Edward Ngoyai Lowassa, aliyekuwa akipeperusha bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Ikiwa leo ni mwaka mmoja tangu kufanyika kwa uchaguzi, watu wengi wameandika vitu tofauti kwenye mitandao ya kijamii wakijikumbusha hali ilivyokuwa ambapo baadhi waliweka picha na video za matukio mbalimbali ya Oktoba 25, 2015.
Aliyekuwa mgombea wa CHADEMA, Edward Lowassa kupitia ukurasa wake wa Facebook na Twitter ameandika ujumbe huu kwa Watanzania.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza mgombea wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi huo na aliapishwa Novemba 2, 2015 kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
UJUMBE ALIOANDIKA EDWARD LOWASSA BAADA YA KUTIMIA MWAKA MMOJA TOKEA SIKU YA KUPIGA KURA
Reviewed by Unknown
on
11:17:00
Rating:
Hakuna maoni: