Mwaimbaji Shaa Aikacha MJ Records, Adai Hayupo Tena Katika Lebo Hiyo Inayomilikiwa na Master Jay
Malikia wa uswazi kama mwenyewe anavyopenda kujiita Shaa ameweka wazi zile tetesi zilizokuwa zimezagaa kwamba ameondoka Mj Record na kesema ni kweli hayupo chini ya lebo hiyo lakini haimaanishi kwa hafanyi kazi na studio za Mj .
Hata hivyo Shaa amesema ameanzisha kampuni yake inayoitwa SK ambayo ni matokeo ya kazi za sugua gaga,toba na nyingine ambazo zilirudisha gharama za Mj na kumuwezesha kufungua kampuni hake hiyo binafsi ambayo anatarajia kusajili wasanii hata wa tano ila kwa sasa yupo yeye peke yake.
Hata hivyo Shaa ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Sawa kupitia kampuni yake hiyo ila unaambiwa Shaa hayupo taari kuyazungumzia mahusiano yake kama ailivyo mpenzi wake Master J ambaye akiulizwa na huwa anajibu lakini kwa Shaa nitofauti kabisaa
Mwaimbaji Shaa Aikacha MJ Records, Adai Hayupo Tena Katika Lebo Hiyo Inayomilikiwa na Master Jay
Reviewed by Unknown
on
04:49:00
Rating:
Hakuna maoni: