MTOTO WA MIAKA 8 ABAKWA NA WAJOMBA ZAKE WATATU

Jeshi la Polisi kwenye jimbo la Nyamira nchini Kenya wamemuokoa mtoto wa kike wa miaka nane ambaye anadaiwa kubakwa na wajomba zake watatu na kuambukizwa ugonjwa wa zinaa.

Binti huyo ambaye anaishi na bibi yake aliokolewa na polisi baada ya jirani kutoa taarifa kwa polisi kuhusu kilichokuwa kinaendelea.

Inaripotiwa kuwa bibi wa mtoto pia anashikiliwa na polisi kwa kosa la kujua kitendo watoto wake walichokuwa wanamfanyia mjukuu wake bila kutoa taarifa polisi.


UKamishna wa Polisi jimboni hapo Isaiah Nakoru ameeleza kuwa washtakiwa hao wanne wanashkiliwa na polisi huku wakisubiri kupelekwa mahakamani huku mtoto akipelekwa idara ya watoto
MTOTO WA MIAKA 8 ABAKWA NA WAJOMBA ZAKE WATATU MTOTO WA MIAKA 8 ABAKWA NA WAJOMBA ZAKE WATATU Reviewed by Unknown on 04:38:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.