TANZIA: Mbunge Mpya wa Cuf Bi Hindu Amefariki Dunia


TANZIA: Bi Hindu Afariki Dunia
Mbunge mteuliwa wa chama cha wananchi (CUF), Bi Hindu Mwenda amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambaya imesema kuwa Bi Hindu amefariki jana jioni baada ya kuugua kwa siku kadhaa japo hajaeleza kiundani chanzo cha kifo chake lakini amesema taratibu nyingine zinazofuata zitaelezwa hapo baadaye.

Marehemu Bi Hindu alikuwa ni miongoni mwa wabunge wapya waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya wabunge nane ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
TANZIA: Mbunge Mpya wa Cuf Bi Hindu Amefariki Dunia TANZIA: Mbunge Mpya wa Cuf Bi Hindu Amefariki Dunia Reviewed by Unknown on 05:45:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.