Taarifa za mvua kubwa kutoka mamlaka ya hali ya hewa (TMA)

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa tahadhari kwa umma kuhusu vipindi vya mvua kubwa vinavyoambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa katika mwambao wa ukanda wa pwani.
TMA katika taarifa yake imetoa tahadhari kuwa, kuanzia leo hadi kesho kutwa kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 vinavyoambatana na upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili.
Mamlaka hiyo imesema maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara. Pia, visiwa vya Unguja na Pemba.
Taarifa za mvua kubwa kutoka mamlaka ya hali ya hewa (TMA) Taarifa za mvua kubwa kutoka mamlaka ya hali ya hewa (TMA) Reviewed by Unknown on 00:25:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.