MWANAMKE WA MIAKA 65 AJIFUNGUA WATOTO WATATU...HEBU MSHUHUDIE HAPA


Mwanamke mwenye umri wa miaka 65 nchini Ujerumani amejifungua watoto watatu baada ya kutunga mimba kwa njia za kupandikiza kisayansi.
Kituo cha runinga cha RTL nchini Ujerumani kimesema mwanamke huyo Annegret Raunigk, amejifungua watoto wawili wa kiume na mmoja wa kike kwa njia ya upasuaji Jijini Berlin.


Watoto hao wamezaliwa kabla ya muda wao wakiwa na wiki 26, hata hivyo madaktari wamesema wote wapo katika hali nzuri ya kuweza kuishi.
Annegret Raunigk ambaye alikuwa na watoto 13 pamoja na wajukuu saba, ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza duniani mwenye umri mkubwa kujifungua mapacha watatu.
MWANAMKE WA MIAKA 65 AJIFUNGUA WATOTO WATATU...HEBU MSHUHUDIE HAPA MWANAMKE WA MIAKA 65 AJIFUNGUA WATOTO WATATU...HEBU MSHUHUDIE HAPA Reviewed by Unknown on 01:09:00 Rating: 5

Hakuna maoni:

Facebook

klin zepp. Inaendeshwa na Blogger.