Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili ameweka wazi kitu cha kipekee kilichomvutia kwa mpenzi wake Joan, hadi kufikia hatua ya kutangaza ndoa.
Akizungumza na www.eatv.tv, Nikki amesema kwamba upendo wa kipekee aliooneshwa na mwanamke huyo ndiyo kitu cha kipekee kilichomnasa, na kufanya awaache wanawake wote warembo bongo na kutua kwake.
“Kwanza ananipenda, hicho ni cha kwanza, lakini cha pili tunaweza kuelewana, ikiwa ni kwenye makosa, kupatia , kuumia, kufurahi, na yeye anaweza kuelewa hapa Niki yupo hivi kwa sababu hii, na ananielewa, lakini pia anaelewa kuwa Nikki ana mazuri yake mengi na mabaya yake, kitu ambacho kinapungukia kwangu anaweza kukijazia,” amesema Nikki.
Nikki wa pili na mpenzi wake Joan wamekuwa kwenye mahusiano kwa zaidi ya miaka miwili, na hivi karibuni ameamua kumchumbia rasmi, ikiwa ni mwanzo wa safari yao ya maisha ya ndoa.
Jumanne, 11 Desemba 2018
Siwezi Kuiposti Familia Yangu Mitandaoni- Ay
AMsanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Ambwene Yesaya maarufu kama ‘AY’ ameibuka na kuweka wazi kuwa kamwe hawezi kuianika familia yake kwenye mitandao ya kijamii.
AY amefunguka na kuweka wazi kuwa moja ya sababu kubwa ya kutoposti picha ya mwanawe na mke wake kwa sasa ni makubaliano kati yao wawili.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA Jumatano, AY alisema haoni sababu ya kufanya hivyo katika mitandao ya kijamii kwa kuwa mwenye jukumu kubwa la kujua familia yake ni yeye peke yake na si watu wengine.
Maisha ya kuposti vitu mitandaoni yakikuingia kichwani ni tatizo sana, ndo ile ikifika wakati humposti wanaanza kuulizana wameachana au, sioni sababu ya kuonyesha kila kitu kwenye maisha yangu, haya ni makubaliano yetu sisi”.
Miezi minne iliyopita AY aliweka wazi kuwa yeye na Mke Wake Remmy walijaliwa kupata Mtoto wao kwanza huko nchini Marekani