Mkali wa muziki wa RnB Bongo, Jux amesema ingawa wameachana na Vanessa Mdee siyo sababu ya kumsema vibaya.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Utaniua’ ameiambia E-Newz ya EATV kuwa analazimika kuwa na nidhamu hiyo kwa sababu kwenye maisha kuna leo na kesho.
“Unajua katika maisha hakuna anayejua kesho kutatokea nini, mimi siwezi kutoa kauli yoyote kwa sababu Vanessa bado nampenda. Tumefanya vitu vingi sana, nampenda na nitaendelea kumpenda kwa kushirikiana kwenye mambo mengi,” amesema Jux.
Katika hatua nyingine alipoulizwa iwapo Vanessa atamfuata na kumtaka warudiane kama atakuwa tayari, Jux alijibu;
“Siwezi nikaliongelea hilo, sijajua kwa hiyo moment itakuwaje, mimi naishi pia siwezi jua kesho nitakutana na nani kitatokea nini, huwezi jua yeye atakutana na nani kitatokea nini, so siwezi nikatoa hilo jibu sasa hivi lakini tuone itakavyokuwa, tunaendelea kuishi you never know,” amesema.
Kipindi cha mapenzi yao waliweza kutoa wimbo wa pamoja uitwao Juu, pia walishirikishwa katika wimbo wa Nikki wa Pili ‘Safari’
Jumamosi, 2 Septemba 2017
Ujumbe mzito wa Shamsa Ford kwa Chidi Mapenzi
Mrembo kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Shamsa Ford ametimiza mwaka mmoja wa ndoa yake na mumewe mfanyabiashara Rashidi Saidi maarufu kama Chidi Mapenzi.
Katika kusherekea mwaka mmoja huo , Shamsa amempa mzito mumuwe kuhusu ndoa yao, yenye mwaka mmoja.
“Leo tumetimiza mwaka mmoja wa ndoa yetu.Tumepitia changamoto nyingi sana kwa muda mfupi wa ndoa yetu ila hatujawahi kuchokana kwasababu Mwenyezi Mungu ndo alituunganisha. Upendo wako kwangu unanifanya nijione mwanamke mwenye bahati duniani na inatosha..Mwenyezi Mungu azidi kutupigania kwenye hii safari ndefu tuliyoianza. Nakupenda, na nakuheshimu sana mume wangu RASHIDI..HAPPY ANNIVERSARY TO US,” ameandika Shamsa katika mtandao wa Instagram.
Shamsa aliolewa mwaka jana Septemba 2, ndoa hiyo iliudhuriwa na watu wa karibu wa mrembo huyo na wa mumewe. Kwa mwaka mmoja wa ndoa ya wawili hao bado hawajabahatika kupata mtoto
TANZIA: Mbunge Mpya wa Cuf Bi Hindu Amefariki Dunia
Mbunge mteuliwa wa chama cha wananchi (CUF), Bi Hindu Mwenda amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambaya imesema kuwa Bi Hindu amefariki jana jioni baada ya kuugua kwa siku kadhaa japo hajaeleza kiundani chanzo cha kifo chake lakini amesema taratibu nyingine zinazofuata zitaelezwa hapo baadaye.
Marehemu Bi Hindu alikuwa ni miongoni mwa wabunge wapya waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya wabunge nane ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba