Alhamisi, 31 Agosti 2017

Hizi Hapa Sababu za Zari Kupungua Mwili Mobetto Atajwa

Hizi Hapa Sababu za Zari Kupungua Mwili Mobetto Atajwa
Mwanamitindo Hamisa Mobeto amedaiwa kuwa sehemu ya kupungua mwili kwa mwanadada mjasiriamali maarufu, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Kwa mujibu wa chanzo makini, tangu Mobeto aanze kuibua mjadala mtandaoni kuhusiana na mtoto wake kudaiwa kuwa ni wa bwana wa Zari, mjasiriamali huyo amejikuta akipungua mwili kutokana na mawazo aliyonayo.

“Zari kapungua mwili kweli jamani. Mobeto amemponza. Amemsababishia watu wamtukane sana Zari kiasi ambacho amekosa amani kabisa. Masikini mtoto wa watu kakonda kweli sasa hivi.

“Ukitazama picha za Zari sasa hivi si Zari yule aliyetoka kujifungua. Tena kwa kawaida tunajua mtu ukitoka kujifungua unanenepa lakini kwa Zari mambo yamekuwa tofauti. Ngoja niwatumie picha yake ya sasa muone,” kilisema chanzo.

Hata hivyo mwanahabari wetu aliingia kwenye ukurasa wa Instagram wa Zari na kujionea jinsi alivyopungua baada ya kuona picha zake mpya na kulinganisha na picha zake za zamani.
Licha ya yeye mwenyewe kutozungumzia suala hilo lakini mashabiki wake walisema amefanya vizuri kujipunguza unene kwani sasa ametokelezea tofauti na zaman

Kweli Pesa Inatakatisha, Huu Ndio Muonekano wa Sasa wa STEVE YANGA (Shabiki wa Yanga wa Kulia lia)


Kweli Pesa Inatakatisha, Huu Ndio Muonekano wa Sasa wa STEVE YANGA (Shabiki wa Yanga wa Kulia lia)
Huyu kijana alijizolea umaarufu miaka ya nyuma kutokana na tabia yake ya kulia lia sana pale timu yake ya Yanga ilipokuwa ikipokea kichapo alikuwa anashindwa kabisa kujizuia vile vile alihangaika kushiriki kwenye mashindano ya bongo star search lakini hakupata nafasi.



Hii picha kipindi analia baada ya yanga kupokea kichapo
hapa kipindi anatafuta nafasi Bongo  Star Search
 Hapa kipindi anatafuta nafasi Bongo  Star Search


Huu sasa ndio muonekano wa sasa baada ya kula kitengo pale AZAM na yanga kawahama kabisa

NB:jamaa mwanzoni alionekana kama kituko sasa hivi kala kitengo hata harmorapa akiendeleza janja janja za kiki atatusua tu siku moja.

“Hakuna Mtu Anayeninunulia Nguo Wala Kunipa Pesa” Agnes Masogange Ataja Sababu Asizoogopa Kuuza Mwili wake

“Hakuna Mtu Anayeninunulia Nguo Wala Kunipa Pesa” Agnes Masogange Ataja Sababu Asizoogopa Kuuza Mwili wake
Aliyekuwa video vixen mkali kutoka Bongo Agnes Masogange amefunguka kuhusu maisha yake huku akigusia kuwa watanzania wengi wanapenda kumponda bure.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Mwanaspoti mrembo huyu alisema Kuwa hana dhiki ikiwa atafikia kiwango cha kuuza mwili wake ili ajitafutie. Masogange alisema,

“Watu bana!, mimi sina dhiki ya kufikia kuuza mwili wangu eti nipate pesa na kuhusu zile picha kipindi kile nilizopiga hazikuwa za utupu sema basi tu watanzania tunapenda kuzusha sana. Na mtu kuenda Sauzi ndio ameenda kujiuza?,” Masogange aliliambia Gazeti la Mwanaspoti.
Aliongeza kuwa hakuna mtu anayemnunulia mavazi anayovaa wala kumpa pesa ya matumizi yake kwa hivyo hakuna anayeweza kumwambia chochote.

“Mimi nilikuwa na biashara zangu nafanya na wanaosema hivyo hawanisaidii chochote,hakuna mtanzania anayeninunulia nguo,hayupo anayenipa pesa waongee tu. Unajua sisi wadada tuna tabia ya kuoneana wivu akiona unafanya vizuri anaanza kukusemea vitu vya ajabu pembeni,”

Ijumaa, 18 Agosti 2017

Video: Huyu ndio msanii wa Afrika Mashariki aliyeamua kumtumia mpenzi wake kwenye video yake

Ni mara chache tumeona wasanii wa muziki wakiwatumia wapenzi wao kama model kwenye video za ngoma zao. Sasa msanii wa Burundi Daddy Face ameamua kumtumia mpenzi wake kama model kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Marry Me’.

Daddy Face akiwa na mpenzi wake wakiwa location wanashoot video
Kitu hicho tumeweza kukiona kwa Diamond alipomtumia Zari kwenye ‘Utanipenda’, Jux alimtumia Vanessa Mdee kwenye video yake ‘Sisikii’, Barnaba na Mama Steve kwenye ‘Wahale’ na nyingine chache.
Msanii huyo wa Burundi ambaye anaishi nchini Marekani ameamua kufanya hivyo kwa madai kuwa anataka kuwaonyesha watu ni kiasi gani anavyompenda mpenzi wake huyo ambaye wamedumu muda mrefu kwenye mahusiano yao bila ya watu wengi kufahamu.
Tazama video hiyo hapa chin

Baba Diamond amshauri mwanaye kuoa wake wawili, Zari na Mobetto

Baba Mzazi wa Msanii Diamond Platinum, Abdul Naseeb amefunguka kuhusu tetesi zinazoendelea za mtoto wake kutajwa kuwa ndiye mzazi halali wa mtoto wa mlimbwende Hamisa Mobeto anayetambulika kwa jina la Abdul Naseeb ambalo ndiyo jina la baba yake na Diamond.
Akizungumza katika kipindi cha SHILAWADU cha Clouds TV Ijumaa hii, Baba Diamond ameeleza kuwa kama Diamond ameamua kumpa mtoto huyo jina lake ni upendo na inaonesha thamani kwake.
Baba Diamond amesema hawezi kumlaumu mwanaye Diamond kwa kilichotokea kwani yeye ni msanii mkubwa anakumbana na vishawishi mbalimbali, hivyo cha kufanya asiendekeze zinaa awaoe wanawake aliozaa nao (Hamisa Mobeto na Zarina Hassan) na awatendee haki kwa kutoa huduma sawa.
Kuhusu wajuukuu zake, Mzee Abdul ameeleza kuwa yeye anawapenda wote ingawa hajawahi kumuona hata mmoja.
Alhamisi hii Diamond aliandika maneno makali mtandaoni yaliyohusishwa kwenda Mobetto ambaye siku chache zilizopita alitangaza jina mwanaye kuwa Abdul Naseeb. Hatua hiyo iliwafanya mashabiki wengi ambao walitaka kumjua baba wa mtoto huyo wa Mobetto kuwa ni Diamond.
Hata hivyo mpaka sasa mkali huyo wa wimbo Eneka hajawahi kutoa neno lolote juu ya mtoto huyo licha ya mama yake pamoja na dada yake Esma kuonekana mara kadhaa wakimtembelea mrembo huyo wakati alipojifungua katika hospitali moja jijiji Dar es salaam

Wanafunzi Wawili wa Shule ya Msingi Wafariki Wakichimba Mchanga wa Kujengea Darasa

Wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Chikomo Tarafa ya Nalasi, Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma wamefariki baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba mchanga wa kujengea darasa walipokuwa kwenye mafunzo ya vitendo.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa ukurasa huu, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa mkoani Rukwa SACP Gemini Mushi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba  wanafunzi waliofariki ni Selina Selemani Kazembe (12) wa darasa la tatu pamoja na Sofia Sillo (9) darasa la tatu kwa kusema kuwa watoto hao waliangukiwa kwa kufunikwa na ukuta wa shimo la mchanga ambao ulikuwa ukitumika kujengea darasa.

Kamanda Mushi amefafanua kwamba "Kwa mujibu wa taarifa tulizopewa na uongozi wa shule hiyo wanafunzi hao walikuwa katika mafunzo ya vitendo yajulikanayo kama elimu ya Kujitegemea (EK).

Pamoja na hayo Kamanda huyo amesema jitihada zilizofanyika ni kuwakimbiza watoto hao katika hospitali ya Mbesa lakini kwa bahatI mbaya wakati watoto hao wanafikishwa hospitali walikuwa wameshakata roho.

Kwa mujibu wa Kamanda Mushi amesema jukumu la mazishi familia hizo zimeachiwa.

TID Ampachika Mimba Mwanamuziki Recho...Mwenyewe Aruka Viunzi...

Msanii Khalid Mohamed maarufu kwa jina la TID, ameruka viunzi na kukana tetesi za kumpachika ujauzito msanii mwenzake Rachel.

Akizungumza kwenye kipindi che eNewz kinachorushwa na East Africa Television, T. I. D amesema kwa sasa hatarajii mtoto yeyote na mwanamke yeyote, na kwamba habari hizo hazina ukweli.

“Hapana, sitarajii mtoto yeyote na Rachel, sina mimba ya Rachel, siyo kweli bwana, hamna mtu mwenye mimba wala nini, kila mtu anataka kuwa na mimba ya Mnyama, sasa wanawake wangapi wanataka kuwa na ujauzito wa mtoto wangu?”, alisikika T. I. D

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa wasanii hao wana mahusiano ya kimapenzi, zilizoibua habari kuwa Rachel ana ujauzito wake

Habari Mbaya Kwa Wanaongalia Video za Ngono Kwenye Simu.....


Hatujaribu kumhukumu mtu yeyote kwa mazoea yake. Kila mmoja ana uhuru wa kutumia simu yake kufanya anachojisikia yeye (hata ikiwa ni kwa kuangalia video za ngono kutoka mtandaoni au zilizohifadhiwa ndani ya kifaa hicho).

Lakini inatakiwa uwe makini kama kuwa unapakua app za bure za ngono kwa kutumia simu yako ya Android, kama ambavyo mtaalamu wa ulinzi mtandaoni wa kampuni ya teknolojia ya Dell, Alex Dubrovsky alipogundua kwamba kuna udukuzi unaofanywa ili kuziathiri app hizo.

Wadukuzi wametengeneza mfumo wa kuiathiri simu unaofichwa ndani ya app hizo ambazo zina uwezo wa kuifunga simu ya mtumiaji na hata kukuzuia usiweze kuifuta app hiyo kutoka kwenye simu yako unapotaka kufanya hivyo.

Dubrovsky na timu yake ya watafiti walmebainisha kuwa wadukuzi wana uhakika kabisa wa kutumia app za ngono kufanya mashambulizi yao: mtumiaji anapakua app na kuwapa wadukuzi njia ya kuingia kwenye simu yako na kuitumia kama ipo kiganjani kwake na kwamba inawapa uwezo wa kufanya chochote. Na kwa wale wanatumia Android toleo la 4.4 KitKat, wadukuzi wanaweza kuifunga kabisa simu yako na kukuzuia usiweze kuifungua tena kama wakitaka.

 “Kutokana na teknolojia ya sasa, ushambuliaji wa aina hii bado unafanywa kwa kiwango kidogo lakini inaelekea utaongezeka kwa kasi kadri muda unavyosonga mbele,” ameandika Dubrovsky. “Kinachoshangaza ni kwamba mpaka sasa, waliofanyiwa udukuzi huu hawajawahi kuombwa pesa ili simu zao zifunguliwet, na pia kwakuwa bado waliokumbana na udukuzi huu wameweza kutumia tena simu zao ni ishara kwamba mfumo huu wa udukuzi haujaanza kutumiwa kwa kiwango cha juu.”

Kwahiyo, ingawa aina hii ya udukuzi bado ipo kwenye hatua za awali ambao kwa sasa walengwa ni watumiaji wa mifumo ya zamani ya simu za Android na kwa kutumia app za ngono pekee, inatabiriwa kuwa baada ya muda udukuzi huu utatumiwa kwenye mifumo ya kisasa zaidi na app nyingine nyingi zaidi (kama wadukuzi wakiweza kupita kwenye mfumo wa ulinzi wa  Google)

Alhamisi, 17 Agosti 2017

Dalili Tano Atakazokuonesha Mwanamke Kama Anataka Kufanya Mapenzi Nawe


Dalili Tano Atakazokuonesha Mwanamke Kama Anataka Kufanya Mapenzi Nawe

1. Kama anazungumzia kuhusu kujamiiana uwapo naye

Kama anaongea kwa kujiamini na ana uhuru wa kutaja mambo mbalimbali yanayohusu kujamiiana kama mkao anaofurahia zaidi wakati wa kujamiiana, vifaa vya vinavyotumika kujiridhisha kingono pamoja na mambo mengine ya kujiridhisha wakati wa kujamiiana, tambua kwamba anataka uendeleze mada hiyo mpaka mjikute mkijamiiana.

Akiamua kuizungumzia kwenye maongezi yenu, yawezekana akawa anakupa ishara kwamba yupo tayari kwa tendo hilo – kilichobaki ni kuomba.

2. Kama ghafla anavaa nguo zinazoacha maungo yake wazi

Njia rahisi ya kumshawishi mwanaume kujamiiana ni pale mwanamke anapovaa nguo za kichokozi, zinazoacha baadhi ya maumbile yake wazi. Kama umezoea kumuona akiwa anavaa nguo rasmi na ghafla akavaa nguo zinazoacha baadhi ya maumbile yake wazi mkiwa kwenye mtoko au miadi yoyote, basi jiongeze – sio lazima akwambie kwakuwa wanawake wengi hawawezi kumwambia mwanaume kuwa anataka wafanye mapenzi.

3. Kama anakualika nyumbani kwake

Baadhi ya wanawake wanapojisikia kufanya mapenzi wanaweza kukualika nyumbani kwake ili mfanye anachokitaka bila kulazimika kukwambia lolote.

Atatandika kitanda, kukupikia chakula unachokipenda au kukupa kinywaji chenye pombe ili ulewe kidogo na kisha muendelee kutokea hapo.

4. Kama anavutiwa na mambo mengi kutoka kwako

Kama anaonesha kuvutiwa zaidi kuliko ulivyozoea siku zote, unatakiwa kujua kwamba yupo tayari kufanya mapenzi na wewe kwa siku hiyo.

Yawezekana akionesha kuvutiwa na wewe kwa kukulegezea sauti au anavyotembea mkiwa mmebaki wawili. Joto la mwili wake linapoongezeka au macho yanapomlegea zaidi. Hii haimaanishi kwamba unatakiwa kumchunguza, ila jaribu kuzingatia kwa makini mabadiliko yanayotokea kuanzia mazungumzo mpaka mwili.

5. Kama anakugusa sehemu zinazokusisimua

Mwanamke anaweza kuamua kukuonesha kuwa yupo tayari kufanya mapenzi na wewe kwa kushika sehemu za mwili wako ambazo zinakusisimua kama masikio, shingo, mapaja, kifua au miguuni.

Baby Madaha Atuhumiwa Kwa Utapeli na Kumloga Jini Kabula Mpaka Kupata Ukichaa

Imasemekena lakini eti, Baby madaha ametapeli pesa za watu. Ni baada ya kukopa nguo na kushindwa kulipa. Pia Baby Madaha na rafiki yake Pichani Isabela wanatuhumiwa kwa kumtengenezea ugonjwa Rafiki yao Kabula, Tuhuma hizi zilitolewa jana na mtangazaji wa U Heard akiwa anamuhoji Isabela live Redioni...Sikiliza Hapa Chini

ALIYEFANIKISHA KUKAMATWA MALKIA WA PEMBE ZA NDOVU KAUAWA KWA RISASI DAR

Mpelelezi kinara aliyefanikisha kukamatwa kwa Yang Feng Glan maarufu kama ‘Malkia wa Meno ya Tembo’Wayne Lotter ameuawa kwa risasi na watu wasiojulikana.
Taarifa iliyochapishwa na mtandao wa The Guardian imesema kuwa Wayne Lotter, 51, alipigwa risasi Jumatano jioni katika maeneo ya Masaki, Dar es Salaam wakati akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo taxi alilopanda lilisimamishwa na gari lingine kabla ya watu wawili kutelemka na kumpiga risasi.
Lotter alikuwa Mkurugenzi na mwanzilishi-mwenza wa PAMS Foundation, Shirika lisilo la Kiserikali ambalo linajihusisha na masuala ya kupinga Ujangili ambalo lilianza shughuli zake Tanzania mwaka 2009 na mara kadhaa amekuwa akipokea vitisho vya kifo.

Mwanajeshi Amvua Nguo Msichana Hadharani Baada ya Kumkuta Amevaa Nguo za Jeshi

Picha inasambaa mitandaoni ikionyesha msichana akivuliwa nguo baada ya msichana huyo kuvaa nguo zinazofanania na sare za jeshi, Haijajulikana ni nchi gani au jeshi gani tukio hili lilipotekea

Wanafunzi 106 watoroka usiku, wavamia sherehe na kupiga watu vibaya

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia wanafunzi 106 wa shule ya Sekondari ya Milambo kwa madai ya kufanya vurugu na kujeruhi wananchi zaidi ya sita katika eneo la jirani na shule hiyo.

Wanafunzi hao wa kidato cha sita wamefanya vurugu hizo usiku baada ya kutoroka shuleni na kuvamia kwenye sherehe ya harusi ambapo walitaka sherehe hiyo iendelee hadi muda watakao amua wao.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa wanafunzi hao 106 wanashikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo

Hatimaye Hamisa Mobetto Amaliza Utata Athibitisha Kuzaa na Diamond

Mobetto Amaliza Utata Athibitisha Kuzaa na Diamondi

Mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobetto Jumatatu hii ametimiza siku saba toka azaliwe Agosti 8 mwaka huu ambapo amepewa jina la Abdul Naseeb. Jina ambalo limeanza kumaliza maswali mengi ya mashabiki ambao walitaka kumjua baba wa mtoto huyo.


Awali mrembo huyo alifungua akaunti ya Instagram kwa jina ‘Tanzania Baby’ lakini Jumanne hii alibadilisha jina na kuandika ‘Abdul Naseeb’ ambapo kwa sasa akaunti hiyo tayari ina wafuasi zaidi 50,000.

Mobetto kupitia Instagram alipost picha yake ya wakati ni ujauzito huku akii-tag akaunti ya mtoto wake huyo na kuandika “Goodnight 😘 .Thank U for this outfit love @fifi_sugardesign . Love U baby dee @abdulnaseeb_tz,”



Wiki iliyopita kupitia kipindi cha Shalawadu cha Clouds TV, mama Diamond pamoja na dada yake Diamond, Esma walionekana katika nyakati tofauti wakiwa katika hospitali moja ambayo alijifungilia mrembo huyo.
Diamond ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul, hajatoa kauli yoyote juu ya mtoto huyo licha tetesi hizo kuonyesha zinaukweli ndani yake.

Kwa sasa muimbaji huyo ambaye ni rais wa WCB, ni baba wa watoto wawili aliozaa na Zari The Bosslady.
Diamond ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul, hajatoa kauli yoyote juu ya mtoto huyo licha tetesi hizo kuonyesha zinaukweli ndani yake.

Kwa sasa muimbaji huyo ambaye ni rais wa WCB, ni baba wa watoto wawili aliozaa na Zari The Bosslady.

Jumatano, 16 Agosti 2017

Hiki ndio Kilichomtia Uchizi Jini Kabula.....Mpaka Kudai yeye ni Ndugu na Rihanna

Msanii wa muziki Issabela Mpanda ambaye ni rafiki wa Karibu wa Mariam Jorwa au jini Kabula ambaye hivi karibuni amepata matatizo ya kurukwa na akili, ameweka wazi kilichomsababishia shoga yake huyo kuchanganyikiwa.


Akizungumza na mwandishi wetu, Issabela amesema daktari ambaye anamtibia Kabula amesema kuwa rafiki yao alikuwa na msongo wa mawazo, lakini kwa sasa yuko sawa.


Pia Issabela ameweka wazi kile ambacho Watanzania wengi walikuwa hawakifahamu kuhusu ugonjwa na matibabu ya Kabula, na kuhusu mtu ambaye amekamatwa kwa kufanya tukio la uhalifu au uvunjaji wa sheria juu ya Kabula.

Jamaa Amuua Mpenzi Wake Kisha na Yeye Kujiua Dar

Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Maria Pius amezikwa leo makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa baada ya mpenzi wake kumuua kwa kumpiga na kitu chenye nchi kali kisha mwili wake kuutupa kwenye shamba huko Chanika jijini Dar es Salaam.

Inasemekana siku ya Jumatatu mwanaume huyo ambaye jina lake halijafahamika alimpiga binti huyo na vitu vyenye ncha kali kwa kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi mpaka alipopoteza maisha kisha muaji huyo aliandika ujumbe unaosema wasimatafute muuaji kwani amemuua yeye, kisha ujumbe huo aliuweka kwenye kifua cha binti huyo pamoja na simu mbili, simu ya mtuhumiwa pamoja na simu ya binti huyo.

Baada ya watu kugundua kuwa binti huyo ameuawa na kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola inadaiwa siku ya kesho yake ambayo ni jana mwanaume huyo aliyedaiwa kufanya mauaji hayo naye aliamua kujitoa uhai kwa kujitumbukiza kwenye kisima cha maji na kupoteza maisha.

Baadhi ya ndugu na majirani wa binti huyo waliopo Mwananyamala sehemu ambayo alikuwa akiishi kabla ya kwenda huko Chanika na kuanza maisha na mwanaume huyo wamesema binti huyo alikuwa anaishi na mwanaume huyo Chanika lakini mwanaume huyo walikuwa hawamfahamu kwani hajawahi kujitambulisha kwao na wala binti huyo hajawahi kumpeleka

PEMBETATU ILIYOGUBIKWA NA MAUZAUZA YA DUNIA YANAYOOGOPESHA BINADAMU


Image may contain: cloud, sky, outdoor, nature and water 

Na Geofrey Chambua
Ikiwa aghalabu unasafiri kwenda Pemba yumkini ufikapo maeneo ya NUNGWI unagubikwa na WOGA, nataka nikubadilishe mawazo kwamba kuna MAENEO YA WOGA ZAIDI DUNIANI 

Bermuda Triangle, ambayo pia inajulikana kama Devil's Triangle, ni eneo la magharibi wa bahari ya Atlantiki ya kaskazini ambapo idadi kubwa ya ndege na vyombo vya baharini vinadaiwa kutoweka katika hali isiyojulikana ambayo haiwezi kuelezewa kama makosa ya binadamu, uharamia, hitilafu ya vifaa, au maafa ya kiasili.


 Tamaduni maalufu zinahusisha kutoweka huku na jambo lisilo la kawaida ambalo haliwezi kuelezewa kwa njia za kisayansi, kutanguliwa kwa sheria za fizikia, au shughuli za viumbe visivyo vya kawaida.Jisomee hapa chini baadhi ya maajabu ya eneo hili

1. Bermuda triangle ni eneo katika uso wa Dunia ambalo linahusishwa na masuala mbalimbali ya nguvu za maajabu, ni eneo ambalo maelfu ya watu wamepoteza maisha, ndege na meli nyingi sana zimezama katika eneo hilo pasipo kujulikana zinaelekea wapi. Wanasayansi wengi wamepoteza pesa zao pasipo kutoa majibu kuhusu maajabu ya eneo hilo na kila aliyeenda hajafanikiwa kutoka na inasemekana Zaidi ya ndege na meli 1000 zimepotea kwa mud wa miaka 500.

2. Bermuda Triangle inapatikana pwani ya kusini mashariki ya marekani na iko katika bahari ya Atlantic. Kona zake huunda pembe tatu ambazo ni Miami huko marekani, San Juan Nchini Puerto Rico na Buermuda katika kisiwa kaskazini mwa kisiwa cha Atlantic.

3. Ajali/mgongano kati ya kimondo na dunia
Inasemekana kuwa Bermuda triangle ilitokea baada ya Dunia kugongana na kimondo huko angani miaka 11,000 iliyopita. Mgongano huo ulitokea katika eneo la bahari la Dunia na kusababisha bahari kuzama kwa futi 10,000 chini ya usawa wa bahari. 


Kimondo hicho kiliacha mionzi ambayo ambayo husababisha ndege kupoteza uelekeo inapofika katika eneo hilo na kuzamsha meli, ndege pamoja na binadamu.
 
4. Viumbe vigeni viishivyo sayari nyingine (aliens).
Inasemekana kuwa viumbe viishivyo angani, huwa vinakaa aktika eneo hilo la Bermuda triangle na hilo ni kama Mecca yao. Viumbe hao wana teknolojia ambayo hukinzana na teknolojia yetu ya Duniani, kwahiyo basi ndege, meli pamoja na binadamu wanapopita pale huvutwa na kani ya uvutano ambayo ni kubwa sana toka kwa wale viumbe waishio katika ilo eneo hilo la bermuda.

5. Kituo cha majaribio ya silaha.
Inasemekana serikali huwa zinajaribia silaha ambazo zinakuwa zimetengenezwa na uangalizi wa silaha hizo, pia inasemekana kwamba serikali ikishirikiana na viumbe watokao sayari (Aliens) zingine huhusika katika majaribio hayo. Na hiyo teknolojia ni kubwa kiasi cha kukinzana na teknolojia ya duniani na hatimaye kusababisha madhara kwa meli na ndege pia.
 
6. Mji uliopotea
Inasemekana katika eneo hilo kulikuwa na mjia wa kale chini ya maji katika bahari ya Atlantic, ulioitwa Atlantis, mji huo ulikuwa umejengeka kwa barafu ambazo zilikuwa kama kioo ambazo pia zilikuwa ni chanzo cha nishati. Na huo mji ulisahaulika milele kwahiyo basi Bermuda iko kwenye huo mji uliozikwa kitambo ambapo kuna kani kubwa ambayo huharibu meli na ndege

7. Kituo cha Maharamia
Inasemekana Bermuda ni eneo kwa ajili ya maharamia kufanya kazi zao, maharamia hao ni wale wanaojulikana kwa bendera nyeusi zenye picha ya fuvu. Lakini dhana hii imeshindwa kuelezea ni kwanini ndege na meli huwa zunapotea katika eneo hilo kwani wachunguzi wa mambo wamehusisha na utekaji nyara wa meli baharini ambao hufanywa na maharamia hao.

8. Volkano.
Inasemekana Volkano pamoja na gesi ya methane katika eneo la Bermuda hupunguza mgandamizo wa maji katika eneo hilo na kufanya meli kupoteza uwezo wa kuelea na hatimaye kuzama. Eneo hilo mlimekuwa likitoa gesi hiyo ya Methane tangu miaka 15,000 iliyopita.

9. Ukungu wenye hali ya ki-electronic na sumaku
Ukungu wenye nguvu ya kuzalisha umeme ambapo husababisha dira hupoteza uelekeo na kuwachanganya marubani pamoja na manahodha. Na hatimaye ndege pamoja na Meli hizo hupotelea katika ilo eneo la Bermuda.

10. Mawimbi na hali ya hewa kubadilika kwa kasi.
Eneo la bahari ya Atlantic hasa upande wa Caribbean hukumbwa na kimbunga kikali pamoja na mawingu mazito, Bermuda ni eneo ambalo limepakana sana na Caribbean na hukabiliwa na upepo na wingu zito ambavyo husababisha mushkeli kwa ndege, meli pamoja na binadamu.

SOKO KUU JIJINI MBEYA SIDO LAUNGUA MOTO

Soko kuu la Jijini Mbeya maarufu kama SIDO limeungua moto usiku wa kuamkia leo .Moto huo ulianza majira ya saa 3 usiku ambapo mali za wafanyabiashara mbalimbali katika soko hilo zimeteketea.

Kwa upande mwingine wananchi wamesikika wakimwaga machozi ya lawama kwa Jeshi la Polisi wakilaumu kutoruhusiwa  kusogea eneo la tukio kuokoa mali zao kwa kuwafyatulia risasi hewani.
Hii ni mara ya tatu sasa ambapo soko hili liliisha ungua mara mbili mfululizo kabla ya  kuungua tena kwa mara nyingine  usiku wa kuamkia leo.

Roma arudi nchini kimya kimya, Aahidi kuweka wazi kila kitu kuhusu ‘Zimbabwe’

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Roma Mkatoliki amewasili jana usiku akitokea nchini Zimbabwe alikoenda kikazi.
Tokeo la picha la Roma mkatoliki
Roma Mkatoliki
Roma Mkatoliki ambaye ameachia wimbo wake mpya wa Zimbabwe wiki iliyopita amejikuta akisakwa na vyombo vya habari kuzungumzia wimbo huo wenye mashairi yenye mafumbo lakini hakuwepo nchini na kumuachia jukumu hilo la kutambulisha wimbo huo kwenye Media, mke wake.
“Kiukweli nimechoka wanangu what i need ni kuona familia yangu, mke wangu na mtoto na ndugu, jamaa na marafiki”,amesema Roma Mkatoliki jana usiku alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. JK Nyerere, jijini Dar es salaam.
Alipoulizwa ni kwanini alimtuma mke wake aachie wimbo huo ile hali alikuwa nje ya nchi Roma Mkatoliki amesema alifanya hivyo kwa sababu muda ulifika wa kutoa ngoma hiyo na tayari alifanya booking na Media, lakini alikataa kuzungumzia wimbo huo wala kueleza alichoenda kufanya Zimbabwe huku akiahidi mashabiki wake kuwa kuanzia leo ataanza Media Tour kuuzungumzia wimbo huo wenye mashairi yenye mafumbo .
Wakazi, Stamina, Ndugu jamaa na Marafiki zake wa karibu wa Roma walikuwepo kwenye mapokezi hayo ambayo yalikuwa kimya kimya

KUPIMA UKIMWI NCHINI ZAMBIA NI LAZIMA SIO HIARI TENA

Rais wa Zambia, Edgar Lungu, ametangaza kwamba wananchi wote wanaofika katika vituo vya afya vya serikali wapimwe virusi vya Ukimwi kwa lazima, wapatiwe ushauri nasaha na tiba.

Rais Lungu amesema, sera hiyo mpya inaenda sawia na agenda ya serikali ya kutokomeza virusi vya HIV nchini humo ifikapo mwaka 2030.

Katika tangazo hilo, kiongozi huyo amesisitiza umuhimu wa kulinda maisha ya wale walioathirika na wale ambao wako hatarini kuambukizwa virusi hivyo.

Amesema, licha ya sera hiyo kukiuka haki ya mtu kupima kwa hiari lakini akasisitiza kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kuweka rehani maisha ya binadamu mwenzake.

Sera hiyo inakiuka muongozo wa Shirika la Afya Duniani, WHO, na Shirika la Ukimwi la Umoja wa Mataifa, UNAIDS, unaohamasisha watu kupima Vvu na kupata ushauri nasaha kwa hiari.

Zambia ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha maambukizi ya ugonjwa huo kusini mwa bara la Afrika ikiwa na asilimia 11.6 huku watu walio na umri wa miaka kuanzia 15 mpaka 49 wakiishi na virusi vya ukimwi.

Bodaboda Wapigwa Marufuku Kubeba Wanafunzi na Watoto Chini ya Miaka 10

Jeshi la Polisi  August 15, 2017 limetoa tamko la kupiga marufuku Waendesha Bodaboda kubeba watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 na kwamba atakayekiuka agizo hilo pamoja na mzazi aliyeruhusu mwanawe kubebwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na faini, kifungo au vyote viwili.

Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Theopista Malya, amesema kuwa watoto wamekuwa kwenye hatari kubwa wakipandishwa kwenye Bodaboda na wakati mwingine waendesha bodaboda hubeba watoto zaidi ya mmoja jambo ambalo ni lazima likemewe.

Aidha, alisema kuwa Jeshi hilo limeandaa kipindi maalumu cha Radio kitakachorushwa na Clouds FM kila siku ya Jumatano saa 2:00 Usiku kikiwa na lengo la kuongeza elimu kwa waendesha Bodaboda katika kuzingatia Usalama Barabarani pindi wanapofanya shughuli zao.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama barabarani (TSA), John Seka alisema kipindi hicho kitalenga kuwapa elimu waendeshaji wa bodaboda.

Pia, alitumia nafasi hiyo kuwataka wafuate sheria zilizowekwa na Sumatra ili waepukane na mkono wa sheria.

Paulina Shayo ambaye ni mwakilishi kutoka WAT Saccos alisema kuwa wanatoa mikopo kwa bodaboda na kwamba mikopo hiyo itawasaidia kuwa wamiliki halali wa vyombo hivyo

Jumatatu, 14 Agosti 2017

Yasome Maneno Haya ya Kanumba Aliyoyaweka Kwenye Blog Yake Siku Chache Kabla ya Kufa



Look at this pic careful,,,moja ya vitu tulivyotofautishwa na wanyama na ndege ni Akili ya kujua mema na mabaya,tizama hao ndege na huyo mbuzi hawana akili kabisa lakini wanapendana ndio maana unaona wako pamoja ILA binadamu aliyepewa akili ana roho mbaya sana,katika mafundisho ya YESU KRISTO alisema neno kuu nawapeni PENDANENI.hata uwe na uwezo wa kuhamisha milima kama huna upendo ni bure,mpende jirani yako kama unavojipenda,upendo 

haujivuni,hauhesabu mabaya,hautakabari,hauhusudu.....nk,1WAKORINTHO 13.Mungu ana akili sana kutuumba kwa mwili huu wa nyama laiti kama angetuumba kwa vioo au sightmirror ili uweze kuona mwenzako anakuwazia nini?anakufanyia nini?anapanga nini juu yako ungekuta ni heri ukaishi msituni na wanyama wakari kuliko kukaa na binadamu,katika tafiti zangu nimegundua kuna dawa mbalimbali mfano ya kichwa,homa,nk Lakini dawa ya Chuki na roho mbaya hakuna,,kama hiki kingekuwa kipindi kama kile cha zamani za Sodoma na Gomora au cha Nuhu ambacho Mungu alikuwa akiadhibu hapo hapo watu wengi sana wangeumbuka hasa wale wanaojifanya wasafi usoni lakini rohoni ni tofauti,Mungu atusaidie sana hasa sisi vijana tujue kusimama katika ukweli na uwazi,tuubebe upendo wa dhati toka rohoni huku mdomoni tukitamka amani ya kweli impendezayo Mungu ili watoto wetu waje watuenzi kwa mazuri na dunia ijivunie uwepo wetu

Inasikitisha Sana..Mwenyekiti wa Kijiji Afia Kifuani mwa BINTI Gesti Akiwa Anachepuka




INASIKITISHA sana! Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkamba Kata ya Kimanzichana mkoani Pwani aliyetambuliwa kwa jina moja la shabani anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 50, anadaiwa kufia kifuani mwa binti mwenye umri wa chini ya miaka 30, wakiwa kwenye gesti moja iliyopo Mzinga-Mbagala jijini Dar.

IJUMAA WIKIENDA LATONYWA

Mara tu baada ya kujiri kwa tukio hilo lililoibua simanzi nzito, Ijumaa Wikienda ambalo huwa halilazi damu kufika eneo la tukio na kuanika kila kitu, lilitonywa na chanzo chake, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo lilifika na kuibuka na mkanda kamili wa sakata hilo. Wawili hao walidaiwa kufika kwenye gesti hiyo na kuomba huduma ya kulala kabla ya kutokea kwa tukio hilo baya.

WALITOKEA KIMANZICHANA

Mwenyekiti huyo alikumbwa na umauti Agosti 11, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa meneja wa gesti hiyo, Hamadi Haji, walipofika, wawili hao walichukua chumba tangu Agosti 8, mwaka huu wakitokea huko Kimanzichana. Meneja huyo aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, baada ya kulipia chumba, wawili hao walikuwa wakifika usiku kulala na mchana walikuwa wakitoka kwenda kwenye mihangaiko yao. “Sijui walikokuwa wakienda, lakini walikuwa wakirudi usiku na kujifungia chumbani.

MSHANGAO

“Lakini katika hali ya kushangaza leo (Ijumaa iliyopita) asubuhi, mwanamke aliyekuwa na mwenyekiti alinifuata na kuniambia mwenzake huyo hamwelewi kwa sababu ghafla alianza kumbadilikia na kukoroma kwa mlio ambao haukuwa wa kawaida.

“Yule mwanamke aliniambia kiongozi huyo alikuwa na dozi fulani aliyopewa baada ya kutoka hospitalini kwa sababu hakuwa vizuri kiafya na hilo ndilo lililowaleta Dar. “Alisema alimkatalia sana wasifanye tendo la ndoa, lakini usiku mzima alikuwa akimlazimisha. “Yule mwanamke alitueleza kuwa baada ya jamaa kumbembeleza sana na kumuongezea na vishawishi vingine, mwanamke alisema alijikuta akilegeza msimamo kisha akamkubalia asije akaona labda hampendi. “Baada ya kumkubalia ndipo wakaanza kufanya yao.

 .
MUUNGURUMO WA AJABU

“Aliendelea kutusimulia kuwa wakati wakiendelea kufanya yao ndipo alipoanza kumsikia mwenzake akitoa muungurumo wa ajabu huku akimng’angania kifuani. “Alitusimulia kuwa alipoona hivyo, akaanza kumshangaa, lakini ghafla alimuona akitupatupa miguu na mikono.

“Alisema baada ya kuona hivyo, alijinasua na kumwangalia mwenzake kwa makini ndipo akamshuhudia akitupatupa mikono na miguu peke yake. “Yule binti alisema kila alipojaribu kumsemesha, jamaa alikuwa hawezi kujibu lolote hivyo alikaa muda fulani akijua mwenzake labda amekumbwa na jambo la kawaida na atarejea kwenye hali yake.

UKIMYA WATAWALA

“Alisema tofauti na matarajio yake, jamaa aliendelea kuwa kimya na hapo ndipo alipoingiwa na hofu. “Alipoona hivyo, ndiyo akaja kunigongea kwenye ofisi yangu. Mimi nikaenda naye kwenye chumba chao kiitwacho Mikumi na kumkuta jamaa amelala kwa staili ambayo hata mimi mwenyewe sikuilewa.

“Ilibidi nimpigie simu mwenyekiti wa serikali ya mtaa wetu, aje tushirikiane kumuangalia,” alisimulia meneja wa gesti hiyo na kuongeza: “Muda mfupi baadaye, mwenyekiti aliwasili na viongozi wenzake na kuingia kwenye hicho chumba ambapo walipomuangalia jamaa, waliniambia kuwa huenda amefariki dunia. “Hapo ndipo wakapiga simu polisi ambao walifika na kuuchukua mwili huo baada ya kugundua jamaa alikuwa amekwishafariki dunia.”


Kufuatia sakata hilo, Ijumaa Wikienda lilifika kwenye ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mzinga A na kumkuta mwenyekiti wa mtaa huo, Chande Mpwati ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo mtaani kwake na kueleza jinsi alivyoshiriki katika kwenda kuukagua mwili wa marehemu na kumuhoji binti aliyekuwa naye.

MAPENZI YA SIRI

Mpwati alisema kuwa, alipomuhoji binti huyo alimwambia kwamba jamaa huyo alikuwa ni mpenzi wake wa siri kwa kuwa ana familia yake kijijini kwao, Mkamba maana mwanamke huyo naye ni mkazi wa huko hivyo walikuja Dar kwa ajili ya mwanaume huyo kutibiwa ambapo walinionesha makaratasi ya hospitalini ndipo umauti ukamfika wakiwa wanafanya mapenzi. “Mwili wake ulichukuliwa na polisi kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Temeke na yule binti alichukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi,” alisema mwenyekiti huyo.

KAMANDA TEMEKE

Ijumaa Wikienda lilizungumza na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, ACP Gilles Muroto ambaye alisema kuwa ishu hiyo ilikuwa haijamfikia mezani kwake, lakini aliahidi kufuatilia kwa watu walio chini yake.