Jumanne, 23 Mei 2017

Vijana wanne wambaka binti wa miaka 15

Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi huku mwingine mmoja akiendelea kutafutwa kwa tuhuma za kumbaka binti mmoja mwenye umri wa miaka 15 wilayani Ilemela, mkoani Mwanza.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kwamba tukio hilo limetokea tarehe 21/05/2017 majira ya saa moja kamili jioni katika maeneo ya mamlaka ya pamba, kata ya Kirumba ambapo inadaiwa kuwa binti huyo ambaye pia ni mkazi wa Kirumba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina moja la Phili na walipanga wakutane katika maeneo hayo.

Inasemekana kuwa binti huyo alikutana na mpenzi wake mahali hapo kisha walikwenda sehemu yenye jumba bovu kuzungumza, wakiwa kwenye eneo hilo ghafla walitokea vijana wengine watatu t\wakishirikiana na Phili na kuanza kumfanyia ukatili kwa kumbaka.

Inasemekana kuwa wakati wakiendelea na ukatili huo binti alipiga yowe akiomba msaada kutoka kwa wananchi, wananchi walifika eneo la tukio na kumuokoa binti na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aitwaye Fredy Remigius kisha walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo.

Askari walifika katika eneo la tukio na kufanya msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wengine huku wakishirikiana na wananchi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine wawili huku mmoja aliyekuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti akifanikiwa kutoroka.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Fredy Remigius miaka 20, mkazi wa Kitangiri, Jackson Joseph miaka 17, mkazi wa Mlimani B na Frank Haruni miaka 18.

Kamanda Msangi amesema mahojiano na watuhumiwa waliokamatwa yanaendelea na pindi uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani na kwamba majeruhi aliyebakwa amepelekwa hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa ajili ya matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Kuhusu shambulio la kigaidi kwenye show ya Ariana Grande mjini Manchester,watu waliofariki…..


Jumatatu ya tarehe 22 May 2017, watu 22 wamefariki dunia kwenye show ya muziki ya msanii Ariana Grande ya “Dangerous Woman” iliyofanyika Manchester Arena mjini Manchester, Uingereza.
CNN wameripoti kuwa watu zaidi ya 54 wamejeruhiwa baada ya mlipuko wa bumo uliotokea kwenye ukumbi wa show hio wenye uwezo wa kujaza watu 21,000.
Ariana aliandika twitter “broken. from the bottom of my heart, i am so so sorry. i don’t have words.
Twit ya Nicki Minaj ilisema “My heart hurts for my sister, Ariana & every family affected by this tragic event in the U.K. Innocent lives lost. I’m so sorry to hear this.
Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha kigaidi ambapo ni mara ya kwanza linatokea tangu lile la mwezi Julai mwaka 2005 ambapo zaidi ya watu 50 walifariki dunia mjini London.
     

Taylor Swift sio SINGLE Tena,huyu ndo baby mpya…


Pop staa Taylor Swift amekuwa mafichoni kwa muda wa miezi mitatu sasa na imegundulika alikuwa studio akitaarisha album yake mpya.
Pia taarifa mpya ni kuwa Taylor Swift ana mpenzi mpya anayetokea Uingereza. Gazeti la #TheSun kuwa Taylor Swift yuko kwenye mahusiano na mwigizaji Joe Alwyn na kwamba Bi Swift hataki waandishi wa habari na mapaparrazi kujua kuhusu mahusiano yake kwa sasa.
Taylor na mpenzi wake wamekuwa walitumia ndege binafsi kwa muda mrefu ili kukaa mbali na mapaparrazi.
Taylor alikimbia macho ya watu baada ya mahusiano yake na DJ Calvin Harris kuvunjika na baadae kutoka na Tom Hiddleston kwa muda mfupi.
Joe Alwyn