Jumapili, 30 Aprili 2017

Nikki Wa Pili azungumzia kauli ya Lord Eyes kuwa Weusi ni Wabinafsi….


Kwenye #FridayNiteLive na #Sammisago mzungumzaji wa kundil Weusi #NikkiWaPili ameongelea kauli ya Lord Eyes kuwa wasanii wa kundi hilo i wabinafsi ndio maana ameshindwa kuendelea kufanya nao kazi.
Nikki amesema “Hio sio kweli na kwamba kama wasanii wa kundi hupeana ushirikiano kwenye kazi na issue zingine, na mtu wa kulalamika kama hivyo ni Bonta ambaye amekuwa nje ya kundi kwa muda kidogo ila sio Lord
#Sammisago -Je kuna masharti yoyote kawekewa Lord Eyes kama anataka kufanya kazi kwenye kundi la Weusi ?
Jibu la #NikkiWaPili – Ndio, kuna ABC amepewa afanye na kama atafanikiwa basi hakuna shida tutaendelea na kazi, hizo ABC siwezi kusema sababu ni siri za kampuni…. 
Je Lord Eyes bado anatumia dawa za kulevya ndio maana bado yupo bechi Weusi ?….Tutafuatilia zaidi

Will Smith kuigiza kama HitMan kwenye filamu mpya,Gemini Man.


Mwigizaji Will Smith yupo kwenye mazungumzo ya kusajiliwa kuigiza kama adui na HitMan kwenye filamu mpya ya Gemini Man.
Filamu hii itaongozwa na mshindi wa tuzo ya Oscar Ang Lee aliyetauarisha filamu kama Crouching TigerHidden Dragon na Brokeback Mountain.
Jerry Bruckheimer aliyeongoza filamu kama Bad Boys na Enemy of the State za Will Smith naye pia atahusika kwenye filamu hii.
Gemini Man ni filamu inayohusu muuwaji atakaye pambana na muwaji mwingine wa kizazi kipya.

Mlinzi wa zamani wa 2 Pac ataja watu waliohusika kwenye kifo cha 2 Pac…ni kutoka kundi gani na kwanini walikuwa na beef nae….

Sababu ya 2Pac kupigwa risasi na ugomvi uliotokea ndani ya ukumbi wa pambano laMike Tyson mjini Las Vegas.
Hii ni kwa mujibu wa mlinzi wa zamani wa 2 Pac na Suge Knight ambaye anasema alikuwepo usiku huo 2 Pac anapigwa risasi.
Blood Piru OG Mob James anasema Kijana kutoka kundi la wahuni la Crips alikanyagwa na 2 Pac walivyokuwa kwenye ukumbi wa MGM Grand mjini Vegas wakati wa pambano la Tyson, 2 Pac hakuomba msamaha na walibadilishana maneno makali, pia Suge Knight hakutaka kuamua ugomvi ndio maana vijana hao waliondka kwa hasira na baadae kumpiga risasi 2 Pac“. 
Blood Piru OG Mob James ambaye alikuwa karibu na Suge Knight boss wa Death Row Records kijana kutoka The South Side Crips ndio alifyatua risasi.
Piru amezidi kulaumu uongozi mbovu wa Suge Knight akidai ata wahuni waliotakiwa kumlinda 2 Pac hawakuwa wanalipwa vizuri na Suge Knight ndio maana ilionekana ni rahisi kumdhuru 2 Pac.
Tupac alipigwa risasi Masaa mawili baada ya kutofautiana na wahuni hao wa Crips, Pac na Suge walikuwa wakielekea kwenye club maarufu ya 662.
Piru anasema Suge Knight ni shetana sababu ata kaka yake alifariki kutokana na yeye kujihusisha na lebo hio ya Death Row na mmiliki wake Suge Knight.

MAHUSIANO:FAHAMU Dalili Za Kuonyesha Kama Imefika muda wa Kumkiss Mpenzi Wako

Lazima uwe mjanja wa kusoma ishara zote kabla hujachukua hatua ya kujaribu kum kiss ama kumla dende mpenzi wako.
Ukijifanya fala wa kuchukua hatua ya haraka kumkiss mpenzi wako kwa mara ya kwanza bila kusoma ishara dhabiti inaweza kukuletea aibu, ama zaidi kukufanya upungukwe na kujiamini kwako wakati mwingine ambao mtakutana tena.
So utafanyaje usipate aibu ama kupungukiwa na kujiamini?
Jambo la msingi ni kuwa lazima nyote wawili muwe mumevutiana aidha kimapenzi ama kuna kemia ya kimahaba ambayo imejijenga kati yenu
Ok. Kuna wengine wangepinga msimamo wangu wa hapo juu ya kuwa si lazima kuwe na mvuto wa kimapenzi kati yenu… Jibu langu ni rahisi. “Unless nyote wawili mumekutana kwa kilabu ama sehemu nyingine na nyote wawili mumeathirika kwa kubugia bia nyingi, haitakuwa jambo zuri kama utachukua hatua ya kumkiss yeyote…mwanzo kumkiss mtu ambaye humjui vizuri kunaweza kuwa matatizo chungu nzima”
So ina haja gani ya wewe kumkiss mtu ambaye humjui? Mbona usimkiss mtu ambaye tayari umemzoea na ambaye kuna tenshen ya kimapenzi kati yenu?
Hoja hii ndio imenifanya nije na:
Dalili za kuonyesha kama imetimia kumla dende mpenzi wako
1. Kabla siku yenu ya kukiss iwadie lazima muwe mumekumbatiana mara kwa mara, mumeweza kugusana na kutomasana sehemu tofauti tofauti hasa kwa mikono, shingo, viganja ama sehemu yeyote ile ambayo nyote wawili mumeona ni sawa. Iwapo hamjawahi kufanya hatua hata moja kama hii, ni bora zaidi usijaribu kuchukua hatua ya kukiss kwani itakujeukia wewe mwenyewe.
2. Kabla hatua ya kukiss haijawaidia, kwa kawaida inatoa wakati ambapo nyinyi wawili mnakaribiana kimwili kuliko kawaida yenu. Mara nyingi wapenzi wawili huanza kugusana mikono, viganja, mgongo au wakati mwingine miguu.
3. Wakati ukifika nyinyi wawili mtakuwa mkiangaliana sana kwa macho huku mkipuuzia mazingira ambayo yamewazunguka. Hatua kama hii ikifika usipoteze muda zaidi.
4. Wakati mwingine ghafla maongezi yenu yanasimama halafu mnaanza kuangaliana machoni kwa muda mrefu kuliko kawaida. Ijapokuwa maongezi yenu yatakuwa yamesimama, hamtaona jambo lolote la kutatanisha bali mtakuwa mnaskia raha na mnavutiana zaidi.
5. Wakati huo mtakuwa mnajiskia mko na raha, na mnaweza kuwa mnacheka sana ama mnatabasamuiana nyote wawili. Ukiona hatua kama hii mpenzi wako anatabasabu na wewe unatabasamu, unaweza kuchukua hatua ya pili ambayo tumeieleza hapo juu.
6. Dalili dhahiri ya kuonyesha kuwa hufai kupoteza hata sekunde moja zaidi ni pale ambapo mpenzi wako ataanza kuonyesha dalili za wazi za kuanza kujilamba midomo yake huku akiiweka unyevu. Pia ukiona akianza kuuma midomo yake huku akiiviringa kwa mitindo flani ni ishara ya kukuambia: “wapoteza muda wangu, nataka unile dende sasa hivi”
7. Mwisho ni kuwa vichwa vyenu vitapinda upande wa kulia huku mkisogeleana. Tenshen ya kimapenzi itakuwa imejijenga kati yenu huku ikikoroga akili na miili yenu. Na mwisho ni ile hatua ya kuyeyusha kiu ambacho kimekuwa kikikuandama tangu siku ulipoweka nuru ya kumwona uliyempenda.

KAJALA Aanika Mwanaume wa Kumuoa..!!

MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja, amefunguka kuwa, endapo ataolewa tena, basi kigezo cha kwanza cha huyo mtarajiwa wake kitakuwa ni kudekezwa.
Kajala ambaye aliolewa kisha ndoa yake kupata matatizo na mumewe kufungwa gerezani na hivi karibuni kuachiwa, alisema endapo itatokea ameolewa kwa mara nyingine basi kigezo cha huyo mwanaume ni lazima awe anayejua kudekeza.
“Nampenda mwanaume mwenye mapenzi ya kweli lakini zaidi ya yote mimi napenda kudekezwa hivyo mwanaume atakayenioa lazima awe na sifa hizo vinginevyo atanisikia kwenye bomba,” alisema Kajala huku akiomba asimzungumzie mumewe ambaye ametoka gerezani hivi karibuni.

Taarifa za mvua kubwa kutoka mamlaka ya hali ya hewa (TMA)

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa tahadhari kwa umma kuhusu vipindi vya mvua kubwa vinavyoambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa katika mwambao wa ukanda wa pwani.
TMA katika taarifa yake imetoa tahadhari kuwa, kuanzia leo hadi kesho kutwa kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 vinavyoambatana na upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili.
Mamlaka hiyo imesema maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara. Pia, visiwa vya Unguja na Pemba.

Ijumaa, 7 Aprili 2017

KUMSAKA MBUNGE WA KAWE HALIMA MDEE KWA KUMTUKANA SPIKA WA BUNGE.

 
Spika wa bunge mhe. Job Ndugai ameagiza jeshi la Polisi kumkamata Mara moja mbunge wa kawe Halima Mdee na kumfikisha bungeni kujibu tuhuma zinazo mkabili za kumtukana Spika.

Ahueni kwa Mdee ni kutekeleza utii wa sheria bila shuruti wa kutumia masaa 24 ya kufika bungeni mwenyewe.

POLISI WATEMBEZA KIPIGO KWA WAUMINI WAKIWA KANISANI NA KUUA MMOJA


Ubalozi wa Marekani nchini Sudan umeukashifu vikali uvamizi wa polisi kwa kanisa moja katika jiji kuu la Khartoum, ambapo mtu mmoja aliuliwa kufuatia mzozo wa ardhi.

Mtu mwingine alijeruhiwa na 13 kutiwa mbaroni katika tukio hilo la tarehe 3 Aprili.

Wafuasi wa kanisa hilo walikuwa wamekaa kidete kwa wiki mbili wakati polisi walishambulia majengo hayo.

Taarifa kutoka kwa Ubalozi wa Marekani ilitaja shambulizi hilo kuwa la unyama na ikasema kuwa wametamaushwa pakubwa na tukio hilo katika shule ya Omdurman Evangelical na Omdurman kanisa Presbyterian 

Ilisema kuwa hatua hiyo ya polisi ilihusishwa na utata wa ardhi na mwekezaji binafsi aliyedai alikuwa amenunua majengo hayo.

Kanisa hilo ambalo linaendesha shughuli za shule hiyo, lilianzishwa na wamishenari kutoka Amerika mwaka wa 1924.

HUYU NDIYE BOSI WA FREEMASON AFRIKA MASHARIKI ALIYEFARIKI DUNIA JIJINI NAIROBI KENYA

Tokeo la picha la freemason sir chande

ALIYEKUWA Kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy’ Chande, amefariki dunia.

Sir Chande amekuwa mwanachama wa Freemason kwa takribani miongo sita tangu ajiunge na umoja huo mwaka 1954.

Kiongozi huyo alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7, 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini mkoani Tabora.

Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii jana asubuhi.

Kulingana na taarifa hizo, kiongozi huyo alifariki dunia jijini Nairobi, Kenya alikokuwa akitibiwa.

NYUMBANI KWAKE
MTANZANIA lilifika nyumbani kwa kiongozi huyo Oysterbay, wilayani Kinondoni jana saa 11 jioni na kukuta geti likiwa limefungwa.

Baada ya waandishi kugonga geti hilo, ndipo alitokea mlinzi na kuwakaribisha ndani, ambako hakukuwa na ishara yoyote kuonyesha eneo hilo kuna msiba wala tukio lolote lisilokuwa la kawaida.

Katika nyumba hiyo kulikuwa na wafanyakazi watatu na walinzi wawili.

Hata hivyo, kabla MTANZANIA halijaondoka nyumbani hapo, alikuja ndugu mmoja wa kiongozi huyo ambaye alithibitishia kuwa ni kweli amefariki dunia.

Ndugu huyo ambaye hakuwa tayari kuandikwa jina lake gazetini kwa madai kuwa si msemaji wa familia, alisema mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumanne jijini Dar es Salaam. 

“Ni kweli mzee amefariki dunia ila mimi si msemaji, familia yote iko jijini Nairobi,” alisema ndugu huyo.

Alisema kiongozi huyo anatarajiwa kuchomwa Jumanne ijayo na kwamba wanatarajia zaidi ya watu 300 kutoka nje na ndani ya nchi watahudhuria mazishi yake.

“Tumeshaanza kufanya ‘booking’ (kukodi) hoteli kwa sababu kutakuwa na ugeni mkubwa utakaokuja kuhudhuria mazishi yake,” alisema. 

Sir Chande alikuwa ni mmoja wa wamiliki wa Shule ya Sekondari Shaaban Robert na pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Makumbusho ya Taifa.

KUJIUNGA FREEMASON
Kiongozi huyo aliwahi kueleza kuwa alijiunga na Freemason Oktoba 25 mwaka 1954 baada ya kupitia usaili.

Aliwahi pia kutunga kitabu alichokiita kwa jina la ‘A night in Africa –journey from Bukene’ (usiku wa Afrika – safari kutoka Bukene).

Katika miaka ya 1950 ndipo alieleza kuanza kutambua kuwa Freemason ipo katika msingi wake, ikiwa ni pamoja na sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu kiimani na kumfanya awe anavyopaswa kuwa.

Aliwahi kuelezea kanuni tatu kubwa za Freemason ikiwa ni pamoja na kumtaka mtu kuwa mkweli na mwenye maadili ambayo hasa Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili ili mwanachama awe mzuri.

Ngazi ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia sanaa na sayansi ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo katika maisha.

Ngazi ya tatu alisema kuwa unafundishwa namna ya kufurahia maisha kwa kiwango chake cha juu kwa kufuata kanuni hizo na mwisho ni upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli.

Katika masha yake aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Shaaban Robert.

Akiwa kwenye Jumuiya ya Freemason katika uhai wake, Sir Chande aliwahi pia kukutana na viongozi mashuhuri nchini kama vile Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, marais wastaafu, Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Hata hivyo kutokana na fikra zilizojengeka katika jamii, Freemason ilikuwa ikiogopwa na kutajwa tajwa na watu vibaya, mojawapo ikiwa ni kupata utajiri kwa njia isiyo ya kawaida.

Hata hivyo, hadi sasa dhana hiyo inaendelea na hakuna lililo wazi katika hili, huku katika mitandao ya kijamii kila mmoja akijadili jumuiya hiyo kadiri anavyoifahamu au kuisikia.

HISTORIA YA SIR CHANDE
Sir Chande alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.

Alifika Tanzania mwaka 1950, alihamia Dar es salaam 1953 na kukutana na watu wengi wa bandarini, shirika la reli na mashirika mbalimbali aliyofanyia kazi.

Katika simulizi zake kadhaa, Sir Chande alisema alikutana na watu wengi ambao walikuwa wanahudhuria vikao vya Freemason, akaanza kuulizia na akajifunza mambo kadhaa kuhusu watu hao.

Wakati huo, hao watu hawakuwa huru kuzungumzia Freemason kama alivyofanya Sir Chande, hasa kabla ya vita ya pili ya dunia.

Sir Chande alisema wakati huo Freemason ilikuwa imegawanywa makundi tofauti, katika hospitali, shule, na mashirika mbalimbali na kulikuwa na kundi maalumu kwa ajili ya matajiri na wafanyakazi wakubwa wa Serikali. Ukiangalia vizuri wengi wao walikuwa ni wazungu na baadhi ya Wahindi.

Kundi la kwanza lilikuwa linaongozwa na watu wa Scotland, makundi mawili yaliyofuata yalikuwa yanaongozwa na Waingereza na kundi la nne lilikuwa linaongozwa na Wahindi ambalo ndilo Chande alilojiunga nalo. Ilimchukua miaka miwili kukubaliwa kujiunga na Freemason.

Aliapishwa rasmi mwaka 1954 akiwa na umri wa miaka 28. Kumbuka kwamba masharti ya kujiunga ni lazima uwe na umri kuanzia miaka 21.

Baada ya hapo ndipo alipanda cheo na kupewa nafasi ya kuongoza kundi au tawi la Freemason katika nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.

Akajiunga na miradi tofauti ya Freemason nchini Uingereza yakiwemo hoteli za kifahari pamoja na kupewa jukumu la kujenga hoteli mpya ya Freemason nchini Ghana kwenye Mji wa Khumasi ambayo ni ya kifahari.

Hoteli nyingine ya kifahari aliyoisimamia ujenzi wake iko Zambia.

Sir Chande anakumbukwa sana kwa kuanzisha shule ya msingi ya Viziwi Buguruni, Dar es Salaam, moja ya taasisi ambazo alizipa kipaumbele mno hadi anaingia kaburini.

Sir Andy Chande alistaafu kama kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki mwaka 2005 baada ya kuifanyia kazi kwa miaka 19, akawa hahudhurii mikutano ya nchi hizi, lakini akishiriki ile ya Uingereza kwa sababu alikuwa akiendelea kufanya kazi na mashirika ya huko.

HISTORIA YA FREEMASON
Freemason ni taasisi kongwe, kubwa na inayotambulika kote duniani.

Pamoja na kwamba shirika hili katika muundo wake wa sasa lilianzishwa mjini London, Uingereza mwaka 1717, lakini historia yake inaelezwa kurudi nyuma katika karne ya 14.

Limekuwa likitajwa kwa kila aina ya minong’ono kiasi kuwa baadhi ya matapeli wamekuwa wakiitumia fursa hiyo kujinufaisha, ikiwamo kutoa matangazo ya kualika watu kujiunga wakilenga kukusanya fedha za ada kwa minajili ya kuwafanya wanachama hao tarajiwa kuwa tajiri, wenye nguvu na ushawishi.

Licha ya marehemu Chande na viongozi wengine duniani kuizungumzia kwa uzuri, lakini bado Freemason inabakia fumbo tata miongoni mwa watu wengi duniani wakiwamo Watanzania.

Kwa mujibu ya vitabu vya historia, Freemason kama neno linavyojieleza kwa Kiingereza, awali lilikuwa kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kwa maneno mengine.

Walikuwa wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki katika zama za kati.

Mejengo mengi ya kale kama vile makanisa, mji wa Rome, Washington DC ilisanifiwa na kujengwa na mafundi hawa ndiyo maana mengi yna alama zao.

Lakini pia vitabu vya historia vinaeleza waashi hawa kutokana na uaminifu wao, walikabidhiwa masuala ya utunzaji fedha za asasi mbalimbali kubwa hasa benki na Kanisa Katoliki.

Wakati wakijenga mahekalu, pia walitengeneza mahandaki ya kuhifadhi fedha na kuzikia.

Utaalamu wao wa ujenzi ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza kupotelea humo ndani usiweze kutoka tena.

Kwa sababu ya kuwa waashi, alama zao kubwa ni vifaa vya ujenzi kama vile pima maji.

Ikatokea kipindi ambapo hawa Freemason wanadaiwa kuasi na kuanza kujishirikisha na mambo ya nguvu za giza, utoaji kafara watu na ushirika na shetani.

Wengine wanasema walianza kuiba fedha za Kanisa Katoliki, lakini ukweli halisi haujulikani.

Kutokana na sababu hizi na nyingine ambazo ni siri kati ya Kanisa na Freemason, wakafukuzwa kutoka ukatoliki.

Ndiyo sababu ambayo inaelezwa kutokuwapo kwa maelewano kati yao na Wakatoliki pamoja na imani nyingine duniani.

Wakatoliki walianzisha shirika jingine badala ya Freemason lijulikanalo kama Jesuits.

Hata hivyo, Freemason ya sasa inaelezwa tofauti na viongozi wake wengi duniani, akiwamo marehemu Sir Chande.

Inajieleza kama taasisi ya kirafiki na kifamilia inayounganisha wanaume wenye tabia nzuri wa dini tofauti, wenye kuchangia imani moja katika ubaba wa Mungu na undugu duniani.

Utamaduni wa Freemason unaanzia wakati wa ujenzi wa hekalu la Mfalme Solomon na sherehe zake za kirafiki hutumia kazi za uashi kuashiria somo la maadili na ukweli.

Uanachama wa Freemason hauingiliani na imani ya mtu, familia au ajira yake na hivyo ni kundi lisilo la kidini wala kisiasa ambalo linakaribisha watu wa imani zote kwa malengo ya kuleta ustawi katika jamii.

AHOJIWA NA KAMATI YA MOI KENYA
Katika miaka ya 1990, Freemason ilipata changamoto kubwa nchini Kenya baada ya Rais, Daniel arap Moi kuunda tume kuchunguza watu wanaoabudu shetani, ambayo moja ya majukumu ya tume yalikuwa kuichunguza Freemason.

“Nilifika mbele ya tume hiyo mara mbili na katika nyakati tofauti kama Mkuu wa Freemason Afrika Mashariki. Nilitoa ushahidi kuhusu kazi tunazozifanya,” alikaririwa Sir Chande akisema wakati huo.

Ijapokuwa tume hiyo haikutoa majibu ya kazi waliyokabidhiwa na Rais Moi, inasemekana ilisafisha tuhuma zilizoelekezwa kwa Freemason.

“Nafurahi kusema kwamba tuhuma zile zilisafishwa zaidi na Rais aliyefuata baadaye, Mwai Kibaki ambaye katika moja ya hotuba zake, alisema Freemason imetoa mchango mkubwa sana nchini Kenya,” Sir Chande aliwahi kukaririwa akisema.

KAZI ZINAZOFANYWA NA FREEMASON
Kazi zinazofanywa sasa hivi na Freemason ni kufundisha wanachama wake kuhusu majukumu yao kwa mwenyezi Mungu, kwa nchi zao, familia, na nchi wanayofanyia kazi hata kama ni ugenini, na kutoa misaada.

UANACHAMA
Duniani kote sasa hivi kuna wanachama milioni 3.5 wa Freemason na wanachangia Dola za Marekani zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya misaada kila mwaka. Kiasi hicho ambacho ni sawa na zaidi ya Dola milioni moja kwa siku, hulenga kusaidia sekta za afya, elimu na wajane wa wanachama wa Freemason, ambao husaidiwa wakiumwa au wakiwa na shida yoyote.

JINSI YA KUJIUNGA
Ili kujiunga ni lazima uwe na umri wa miaka 21, ni hiari kujiunga na pia uwe unamwamini Mungu, haijalishi ni Mungu gani. Watu ambao hawamwamini Mungu hawaruhusiwi kuwa Freemason, na lazima uwe mtu mkweli.

Ni lazima familia yako ikubali pia wewe kujiunga na Freemason kwa sababu jumuiya hiyo haitokubali kujiunga kwako kukufanye uwe masikini kutokana na kutoa misaada.

Unapotaka kujiunga ni lazima upeleke maombi yako kwa mtu unayemfahamu ambaye yuko Freemason, au kama hujui mtu unaandika barua na baada ya hapo utapewa nakala za kusoma na kuelewa na kamati ya kukuruhusu kuingia itakupeleleza wewe na familia yako, na pia watakutembelea nyumbani kuongea na mkeo au mumeo au familia.

Inaweza kuchukua mwaka mmoja hadi mwaka mmoja na nusu kuruhusiwa kujiunga na Freemason baada ya kupeleka maombi.

Kuna vyeo vitatu ambavyo huitwa digrii ambavyo ni lazima uvikamilishe jambo ambalo linaweza kuchukua zaidi ya miaka miwili.

BAADA YA KUJIUNGA
Pia unatakiwa kujifunza vitu vingi na kuvihifadhi kichwani kama vile maneno ya kusema wakati unafanya ibada za Freemason kwa sababu unavyozungumzia sifa za kuwa binadamu kamili unaweza ukafananisha na ibada ya kanisani.

FAIDA
Hakuna faida za kupata pesa kama wengi wanavyoambiwa kwamba ukiwa Freemason unapewa fedha nyingi, faida zake ni pamoja na kuongeza idadi ya marafiki na kuongeza ufahamu.

Faida nyingine labda ni kama unaanzisha kiwanda na umetoa tenda ya kazi, ukiona mmoja wa Freemason yuko kwenye orodha ya walioomba tenda utampa kipaumbele kwa sababu unamfahamu na ni kama ndugu.

Hakuna utoaji wa kafara kama inavyosemekana na pia hakuna uhusiano kati ya Freemasons na agano la kale.

Jumatano, 5 Aprili 2017

RAIS MSTAAFU KIKWETE AVUNJA REKODI YA KUSHANGILIWA BUNGENI LEO..ONA ILIVYOKUWA


VIFIJO , vigeregere na nderemo vimetawala bungeni baada ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Kikwete ambaye alimsindikiza mkewe,  alitambulishwa mara baada ya mkewe Salma Kikwete kuapishwa kuwa Mbunge wa Kuteuliwa.

Baadhi ya wabunge walisikika wakisema "tumekumiss tumekumiss" huku wengine wakisema apewe awamu nyingine ya kuongoza.

Wengine walitaka Kikwete aruhusiwe  kuwahutubia jambo ambalo lilishindikana kwa wakati huo kutokana na sababu za kikanuni, ambapo kabla ya kuruhusiwa kuhutubiwa ilitakiwa kanuni zitenguliwe kwanza.

Spika Ndugai alijaribu kuwatuliza wabunge lakini ilishindikana waliendelea kushangilia huku wakiimba wimbo mpya wa Nay wa Mitego wa 'Wapo'.

Spika Ndugai alichagiza kwa kusema, katika historia ya Bunge haijawahi tokea mgeni akashangiliwa kama ilivyotokea kwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na kwamba hii imevunja rekodi.

Baada ya muda Spika aliwasihi wabunge kunyamaza ili shughuli za bunge ziendelee.

Kikwete akiwa na wasaidizi wake pamoja na mwanawe Ali waliondoka kupisha shughuli za Bunge ziendelee kwani angeendelea kuwemo bungeni utulivu ungeendelea kutoweka.

Jumanne, 4 Aprili 2017

Polisi Yaua Majambazi Yakiume Yaliyokuwa Yamevaa Hijabu

Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi  wameuwa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kukaidi amri ya kutakiwa kusimama eneo la kizuizi cha Mwembe Muhoro wilayani Rufiji, mkoani Pwani.

Watu hao walikuwa wamepakiana kwenye pikipiki moja huku wakiwa wamevaa hijabu.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, kamanda wa Polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga alisema pikipiki nyingine mbili zilifanikiwa kukimbia.

Akielezea juu ya tukio hilo alifafanua,lilitokea Aprili 2 mwaka huu majira ya mchana ,Muhoro ,Rufiji barabara kuu ya Dar es Salaam Lindi.

“Siku ya tukio askari walipata taarifa kuwa kulikuwa na pikipiki tatu zikitokea Kibiti kwenda mikoa ya Kusini zikiwa zimebeba watu watatu kila moja “

“Miongoni mwa pikipiki hizo kati yake mbili wamebebwa watu waliovaa hijabu,” alisema Lyanga.

Alisema askari wa barabarani walipewa taarifa katika kizuizi cha Mparange na kuwasimamisha ili wawahoji lakini walikataa na kupita ambapo waliwajulisha wenzao kwenye kizuizi cha Ikwiriri lakini walikaidi kusimama.

“Baada ya hapo walifika kizuizi cha Ikwiriri lakini bado walikaidi kusimama na kuendelea kukimbia ndipo walipofika kituo cha Muhoro “

“Hata hivyo hawakusimama na askari waliokuwa doria wakiwa kwenye gari waliwafuatilia na wakavuka daraja la Mkapa na waliwapa onyo kwa kupiga risasi hewani,” alisema Lyanga.

Aidha alibainisha baada ya hapo watu hao waliruka kwenye pikipiki na kuanza kukimbilia msituni na ndipo askari walipowapiga risasi za miguu na kiunoni na kufanikiwa kuwakamata.

“Majeruhi hao walijulikana ni wanaume hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika na walikuwa kwenye pikipiki yenye namba za usajili MC 272 BLW aina ya Boxer yenye rangi nyeusi”

“Watu hao wanaodhaniwa kuwa ni majambazi  kwa mwonekano wao walijaribu kuwawahisha hospitali ya Misheni ya Mchukwi,” alisema Lyanga.

Lyanga alisema walipofikishwa hospitali daktari alithibitisha kuwa watu hao wamefariki dunia .

Hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika huku pikipiki nyingine mbili zilitoroka na kuelekea mkoa wa Lindi na taarifa zimetolewa polisi ili wawakamate.

Aliwataka wananchi kuwa watulivu pale wanaposimamishwa na askari polisi badala ya kujaribu kutoroka na kwa sasa jeshi hilo limeimarisha doria katika kukabiliana na uhalifu

Meneja wa Diamond Platinumz, Babu Tale na Erick Shigongo Ndani ya Bifu Zito

Mgogoro ulioanza kufukuta kwenye mitandao ya kijamii kati ya mmiliki wa makampuni ya Global Publishers, Erick Shigongo na meneja wa Diamond Platinumz, Babu Tale umechukua sura mpya  baada ya meneja huyo kudai ametishiwa.

Mtafaruku kati ya wawili hao ulianza baada ya Shigongo kuandika katika ukurasa wake wa Instagram ushauri wake kwa Diamond akidai kuwa kitendo cha kujikita katika matamasha ya kimataifa na kuyaweka kando ya ndani huku akitaka kulipwa zaidi ya shilingi milioni 100 pia ndani ya nchi kutamgharimu hususan kupoteza mashabiki wa ndani siku za usoni.

Akifunguka jana kupitia ‘Shilawadu’ ya Clouds TV, Babu Tale ambaye alimtaja Shigongo kuwa ni mtani wake kikabila, alimlalamikia kwa kudai kuwa alimpigia simu na kumweleza maneno ambayo aliyatafsiri kama vitisho.

Alidai kuwa baada ya kumpigia simu na mwandishi huyo nguli wa vitabu vya uhamasishaji wa kiuchumi na masimulizi alimuuliza ‘kama anataka vita’ kati yao baada ya maelezo.

“Nikipata matatizo leo,  ina maana aliyeniambia ‘ninataka vita’ ina maana amenisababishia matatizo. Lakini sitaishia hapa nitafuata vyombo vya sheria ili vinilinde,” alisema Babu Tale.

Meneja huyo wa WCB alionesha kushangazwa na kitendo cha Shigongo kumshauri Diamond kupitia Instagram, akidai kuwa kama angekuwa na nia njema kweli angemuita na kumshauri hata akiwa ofisini kwake.

Tale alienda mbali na kueleza kuwa Shigongo anampango wa kumuangusha katika biashara zake baada ya wawili hao kushindwana katika mambo yao ya kibiashara. Alimlaumu Shigongo pia kwa kuweka hadharani ujumbe aliomtumia kwenye simu.

Bado haijajulikana uhalisia wa chanzo cha mgogoro huo, lakini dalili zote zinaonesha huenda kukawa na msuguano wa kibiashara au kutoelewana katika hoja dhidi ya Diamond Platinumz ambaye ni bidhaa kubwa Afrika iliyo kwenye mikono ya Babu Tale na Salaam.

Jumapili, 2 Aprili 2017

Haya Ndio Maajabu ya Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka Huu..!!!!


Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 zimezinduliwa rasmi leo katika uwanja wa Kumbukumbu Mjini Mpanda mkoani Katavi na unatarajiwa kuzunguka katika mikoa yote 31, ukipita kwenye halmashauri 195 kwa muda wa siku 195.

Katika sherehe hizo za uzinduzi, kiongozi wa mbio hizo kwa mwaka huu pia ametangazwa rasmi, ambapo atakuwa ni Amour Amad Amour kutoka mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar.

Kiongozi huyo atasaidiana na wenzake watano katika kukimbiza mwenge huo ambao ni pamoja na Bahati Mwaniguta Lugodisha (Geita), Bi Fatima Yunus Hassan (Kusini Pemba), Fredrick Joseph (Singida), Salome Obadia Mwakitalima (Katavi) na Shukran Islam Msumi (Mjini Magharibi).

Kauli mbiu ya mbio hizo kwa mwaka huu inasema "SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU'

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kwa niaba ya Rais wa serikali hiyo Dkt. Ali Mohamed Shein, ambapo katika ujumbe wake amesisitiza umuhimu wa watanzania wote kuweka nguvu zao katika kujenga taifa la viwanda

Amesema hadi sasa tangu serikali yake iingie madarakani kwa muhula wa pili tayari viwanda vitatu vya watu binafsi vimekwishajengwa visiwani Zanzibar

Balozi Seif amesema mbali na kaulimbiu ya mwaka huu kusisitiza umuhimu wa viwanda, pia mbio hizo zitakuwa zikieneza ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya Malira, UKIMWI, Dawa za Kulevya pamoja na rushwa.

Mbio hizo zimeanzia katika wilaya ya Mpanda, na kilele chake kitakuwa ni Oktoba 14 katika mkoa wa Mjini Magharibi.

Kumbukumbu zinaonesha tukio kama hili la uzinduzi tangu mwaka 2011 lilikuwa kama ifuatavyo

2011 Butiama (Mgani rasmi akiwa Mohamed Ghalib Bilal)
2012 Mbeya (Mgeni rasmi akiwa Mizengo Pinda)
2013 Pemba (Mgeni rasmi akiwa Dkt Ali Mohamed Shein)
2014 Kagera (Mgani rasmi akiwa Mohamed Ghalib Bilal)
2015 Ruvuma (Mgeni rasmi akiwa Dkt Ali Mohamed Shein)
2016 Morogoro (Mgeni rasmi akiwa Samia Suluhu Hassan)